Biblia inasema nini kuhusu Baali – Mistari yote ya Biblia kuhusu Baali

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Baali

Waamuzi 2 : 23
23 Basi BWANA akawaacha mataifa yale, wala hakuwafukuza kwa upesi, wala hakuwatia katika mikono ya Yoshua.

1 Samweli 7 : 4
4 Ndipo wana wa Israeli wakayaondoa Mabaali na Maashtorethi, wakamtumikia BWANA peke yake.

2 Wafalme 17 : 16
16 Wakaziacha amri zote za BWANA, Mungu wao, wajitengenezea sanamu za kusubu, yaani, ndama wawili, wakafanya na Ashera, wakaliabudu jeshi lote la mbinguni, wakamtumikia Baali.

Yeremia 23 : 13
13 ① Nami nimeona upumbavu katika manabii wa Samaria; walitabiri kwa Baali, wakawakosesha watu wangu Israeli.

Hosea 13 : 1
1 ⑳ Efraimu aliponena, palikuwa na tetemeko; alijitukuza katika Israeli; Lakini alipokosa katika Baali, alikufa.

1 Wafalme 16 : 33
33 Ahabu akaifanya Ashera; Ahabu akazidi kumghadhibisha BWANA, Mungu wa Israeli, kuliko wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.

1 Wafalme 18 : 18
18 Naye akajibu, Si mimi niliyewataabisha Israeli; bali ni wewe, na nyumba ya baba yako, kwa kuwa mmeziacha amri za BWANA; nawe umewafuata mabaali.

1 Wafalme 19 : 18
18 ⑦ Pamoja na hayo nitajisazia katika Israeli watu elfu saba, kila goti lisilomwinamia Baali, na kila kinywa kisichombusu.

2 Wafalme 3 : 2
2 ① Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA; ila si kama baba yake na kama mama yake; maana akaiondoa ile nguzo ya Baali aliyoifanya baba yake.

2 Wafalme 21 : 3
3 ⑲ Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia.

2 Mambo ya Nyakati 22 : 4
4 Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA kama nyumba ya Ahabu; kwa kuwa hao walikuwa washauri wake, baada ya kifo cha baba yake, hata aangamie.

2 Mambo ya Nyakati 24 : 7
7 ⑩ Kwa kuwa wana wa Athalia, yule mwanamke mwovu, walikuwa wameibomoa nyumba ya Mungu; na vitakatifu vyote vya nyumba ya BWANA wamewapatia Mabaali.

2 Mambo ya Nyakati 28 : 2
2 ⑳ bali akaziendea njia za wafalme wa Israeli, alitengeneza sanamu za mabaali za kusubu.

2 Mambo ya Nyakati 33 : 3
3 Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopabomoa Hezekia babaye; akazisimamisha madhabahu za Mabaali, akafanya sanamu za Maashera, akaabudu jeshi lote la mbinguni, na kulitumikia.

Yeremia 2 : 8
8 Makuhani hawakusema, Yuko wapi BWANA? Wala wanasheria hawakunijua; wachungaji nao waliniasi, nao manabii walitoa unabii kwa Baali, wakafuata mambo yasiyofaidia kitu.

Yeremia 2 : 23
23 Wawezaje kusema, Sikutiwa unajisi, sikuwafuata Mabaali? Itazame njia yako bondeni, ujue uliyoyatenda; wewe u ngamia mwepesi, apitaye katika njia zake;

Yeremia 7 : 9
9 ⑭ Je! Mtaiba, na kuua, na kuzini, na kuapa kwa uongo, na kumfukizia Baali uvumba, na kuifuata miungu mingine ambayo hamkuijua;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *