Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Astronomia
Ayubu 26 : 7
7 ⑯ Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Na kuutundika ulimwengu pasipo kitu.
Ayubu 26 : 13
13 ⑳ Hizo mbingu hupambwa kwa roho yake; Mkono wake umemchoma nyoka aendaye mbio.
Ayubu 37 : 18
18 Je! Waweza kuzitandaza mbingu pamoja naye, Ambazo zina nguvu kama kioo cha kuyeyushwa?
Ayubu 38 : 33
33 ⑧ Je! Unazijua amri zilizoamriwa mbingu? Waweza kuyathibitisha mamlaka yake juu ya dunia?
Zaburi 8 : 3
3 ⑰ Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha;
Zaburi 19 : 6
6 Kuchomoza kwake ni katika mwisho wa mbingu, Na kuzunguka kwake ni hadi miisho ya mbingu, Wala hakuna kitu Kisichofikiwa na joto lake.
Zaburi 68 : 33
33 Apandaye mbingu za mbingu za tangu milele; Aitoa sauti yake, sauti ya nguvu.
Zaburi 136 : 9
9 Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Isaya 13 : 10
10 ③ Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
Isaya 40 : 22
22 Yeye ndiye anayeketi juu ya duara ya dunia, na hao wanaokaa ndani yake huwa kama panzi; yeye ndiye azitandazaye mbingu kama pazia na kuzikunjua kama hema ya kukaliwa;
Isaya 40 : 26
26 Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.
Isaya 47 : 13
13 Umechoka kwa wingi wa mashauri yako; basi, na wasimame hao wanajimu, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe kutoka kwa mambo yatakayokupata.
Yeremia 31 : 37
37 ⑲ BWANA asema hivi, Kama mbingu zikiweza kupimwa, na misingi ya dunia ikiweza kugunduliwa huko chini, ndipo wazao wa Israeli pia nitawatupilia mbali, kwa ajili ya hayo yote waliyoyatenda, asema BWANA.
Yeremia 33 : 22
22 Kama vile jeshi la mbinguni haliwezi kuhesabiwa, wala mchanga wa bahari kupimwa; ndivyo nitakavyoongeza wazao wa Daudi, mtumishi wangu, na Walawi wanaonihudumia.
Amosi 5 : 8
8 ⑭ mtafuteni yeye afanyaye Kilimia na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; BWANA, ndilo jina lake;
1 Wakorintho 15 : 41
41 Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota.
Yoshua 10 : 14
14 Haikuwapo siku nyingine mfano wa siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizofuata baada yake, hata ikawa yeye BWANA kuisikia sauti ya binadamu; kwa kuwa BWANA alipiga vita kwa ajili ya Israeli.
Ayubu 9 : 9
9 Yeye afanyaye hizo nyota za Dubu, na Orioni, na hicho Kilimia, Na makundi ya nyota ya kusini.
Mhubiri 1 : 5
5 Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake.
Isaya 13 : 13
13 ④ Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya BWANA wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali.
Isaya 34 : 4
4 Na jeshi lote la mbinguni litafumuliwa, na mbingu zitakunjwa kama karatasi, na jeshi lao lote litanyauka kama vile jani la mzabibu linyaukavyo na kupukutika, na kama jani la mtini linyaukavyo na kupukutika.
Ezekieli 32 : 8
8 Mianga yote ya mbinguni iangazayo nitaifanya kuwa giza juu yako, nami nitatia giza katika nchi yako, asema Bwana MUNGU.
Mathayo 24 : 29
29 Lakini mara tu, baada ya dhiki ya siku zile, jua litatiwa giza, na mwezi hautatoa mwanga wake, na nyota zitaanguka kutoka mbinguni, na nguvu za mbinguni zitatikisika;
Marko 13 : 25
25 Na nyota za mbinguni zitakuwa zikianguka, na nguvu zilizo mbinguni zitatikisika.
Mathayo 24 : 35
35 ③ Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Mathayo 27 : 45
45 Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hadi saa tisa.
Leave a Reply