Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia asali
Isaya 7 : 15
15 Siagi na asali atakula, wakati ajuapo kuyakataa mabaya na kuyachagua mema.
Kutoka 3 : 8
8 ⑫ nami nimeshuka ili niwaokoe kutoka kwa mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hadi nchi njema, kisha pana; nchi itiririkayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.
Mathayo 3 : 4
4 ⑥ Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
Mithali 25 : 27
27 Haifai kula asali nyingi mno; Vile vile mtu kutafuta utukufu wake mwenyewe si utukufu.
2 Samweli 17 : 29
29 ⑮ na asali, na siagi, na kondoo, na samli ya ng’ombe, wapate kula Daudi na watu waliokuwa pamoja naye; kwani walisema, Watu hao wanaona njaa, tena wamechoka, nao wana kiu huku nyikani.
Mithali 24 : 13
13 Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo.
Zaburi 81 : 16
16 Naam, ningewalisha kwa ngano iliyo bora zaidi, Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani.
Wimbo ulio Bora 4 : 11
11 ③ Bibi arusi, midomo yako yadondosha asali, Asali na maziwa viko chini ya ulimi wako; Na harufu ya mavazi yako Ni kama harufu ya Lebanoni.
Zaburi 19 : 7 – 11
7 Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia hekima mtu asiye nayo.
8 Maagizo ya BWANA ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya BWANA ni safi, Huyatia macho nuru.
9 Kicho cha BWANA ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za BWANA ni kweli, Zina haki kabisa.
10 Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali.
11 Tena mtumishi wako huonywa kwazo, Katika kuzishika kuna thawabu kuu.
1 Samweli 14 : 25
25 Nao watu wote wakaingia mwituni; na humo mlikuwa na asali juu ya nchi.
Kutoka 16 : 31
31 ⑬ Na nyumba ya Israeli wakakiita jina lake Mana; nacho kilikuwa mfano wa chembe za mtama, nyeupe; na utamu wake ulikuwa kama utamu wa maandazi membamba yaliyoandaliwa kwa asali.
Ezekieli 27 : 17
17 ③ Yuda, na nchi ya Israeli, walikuwa wachuuzi wako; walitoa badala ya bidhaa yako ngano ya Minithi, na mtama, na asali, na mafuta, na zeri.
2 Wafalme 18 : 32
32 ⑰ hata nije nikawachukue mpaka nchi iliyo kama nchi yenu wenyewe, nchi ya nafaka na divai, nchi ya chakula na mashamba ya mizabibu, nchi ya mafuta ya mzeituni na asali, ili mpate kuishi, msife; wala msimsikilize Hezekia, awadanganyapo, akisema, BWANA atatuokoa.
Mambo ya Walawi 20 : 24
24 ⑪ Lakini mimi nimewaambia ninyi, Mtairithi nchi yao, nami nitawapa ninyi kuimiliki; nchi iliyojaa maziwa na asali; mimi ni BWANA, Mungu wenu, niliyewatenga ninyi na mataifa.
Mambo ya Walawi 2 : 11
11 Sadaka ya unga yoyote itakayosongezwa kwa BWANA isitiwe chachu kabisa; kwa kuwa hamtateketeza chachu, wala asali yoyote, kuwa ni sadaka ya kusongezwa kwa BWANA kwa njia ya moto.
Kumbukumbu la Torati 6 : 2 – 3
2 upate kumcha BWANA, Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria zake, ninazokuamuru, wewe na mwanao, na mwana wa mwanao, siku zote za maisha yako; tena siku zako ziongezwe.
3 Sikiliza basi, Ee Israeli, ukaangalie kuzitenda; upate kufanikiwa, mpate kuongezeka sana, kama BWANA, Mungu wa baba zako, alivyokuahidi, katika nchi ijaayo maziwa na asali.
Ezekieli 3 : 1 – 3
1 ⑤ Akaniambia, Mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha nenda ukaseme na wana wa Israeli.
2 Basi nikafunua kinywa changu, naye akanilisha lile gombo.
3 Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali.
Mithali 25 : 16
16 Je! Umeona asali? Kula kadiri ya kukutosha; Usije ukashiba na kuitapika.
2 Mambo ya Nyakati 31 : 5
5 Mara amri ilipovavagaa, wana wa Israeli wakatoa kwa wingi malimbuko ya nafaka, divai, mafuta, asali, na mazao yote ya mashamba; na zaka za vitu vyote wakazileta kwa wingi.
Ezekieli 20 : 6
6 katika siku ile niliwainulia mkono wangu, kuwatoa katika nchi ya Misri, na kuwaingiza katika nchi niliyowapelelezea, itiririkayo maziwa na asali, ambayo ni utukufu wa nchi zote;
Leave a Reply