Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Antiokia
Matendo 11 : 30
30 Wakafanya hivyo, wakawapelekea wazee kwa mikono ya Barnaba na Sauli.
Matendo 13 : 1
1 ② Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri,[2] na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kulelewa wa mfalme Herode, na Sauli.
Matendo 14 : 27
27 ⑭ Hata walipofika wakalikutanisha kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwamba amewafungulia Mataifa mlango wa imani.
Matendo 14 : 28
28 Wakaketi huko wakati usiokuwa mchache, pamoja na wanafunzi.
Matendo 15 : 35
35 Na Paulo na Barnaba wakakaa huko Antiokia, wakifundisha na kulihubiri neno la Bwana, pamoja na watu wengine wengi.
Wagalatia 2 : 15
15 Sisi tulio Wayahudi kwa asili, wala si wa Mataifa wenye dhambi,
Matendo 13 : 52
52 Lakini wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.
2 Timotheo 3 : 11
11 ⑯ na upendo, na subira; tena na adha zangu na mateso, mambo yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Listra, kila namna ya adha niliyoistahimili, naye Bwana aliniokoa katika hayo yote.
Matendo 14 : 22
22 ⑪ wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwahimiza wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi.
Matendo 18 : 22
22 na alipokwisha kushuka Kaisaria, akapanda juu, akawasalimu kanisa, kisha akateremka kwenda Antiokia.
Leave a Reply