Biblia inasema nini kuhusu Anthropomorphisms – Mistari yote ya Biblia kuhusu Anthropomorphisms

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Anthropomorphisms

Mwanzo 2 : 3
3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.

Kutoka 31 : 17
17 ⑦ Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, akapumzika kwa siku ya saba na kustarehe.

Mwanzo 2 : 19
19 ① BWANA Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.

Mwanzo 6 : 6
6 BWANA akaghairi kwa kuwa amemwumba mwanadamu duniani, akahuzunika moyo.

Kutoka 32 : 14
14 Na BWANA akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake.

Waamuzi 2 : 18
18 ⑭ Na kila wakati BWANA alipowainulia waamuzi, ndipo BWANA alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana BWANA alisikitishwa na kilio chao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua.

1 Samweli 15 : 35
35 Wala Samweli hakuenda tena kuonana na Sauli hata siku ya kufa kwake; lakini Samweli alikuwa akimlilia Sauli; naye BWANA akaghairi ya kuwa amemtawaza Sauli awe mfalme juu ya Israeli.

2 Samweli 24 : 16
16 ③ Lakini huyo malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili auharibu, BWANA akaghairi katika mabaya, akamwambia huyo malaika mwenye kuwaharibu watu, Yatosha, sasa ulegeze mkono wako. Naye yule malaika wa BWANA alikuwako karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna,[20] Myebusi.

1 Mambo ya Nyakati 21 : 15
15 Naye Mungu akatuma malaika aende Yerusalemu ili auangamize; naye alipokuwa tayari kuangamiza, BWANA akatazama, akaghairi katika mabaya, akamwambia malaika aharibuye, Basi yatosha; sasa ulegeze mkono wako. Naye malaika wa BWANA akasimama karibu na kiwanja cha kupuria cha Arauna,[19] Myebusi.

Zaburi 106 : 45
45 ③ Akawakumbukia agano lake; Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;

Yeremia 26 : 19
19 ⑰ Je! Hezekia, mfalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda, walimwua Mikaya? Je! Hakumcha BWANA, na kumwomba BWANA awafadhili; naye BWANA akaghairi, asiyatende mabaya yale aliyoyatamka juu yao? Lakini sisi tuko karibu kujiletea maafa makuu wenyewe.

Amosi 7 : 3
3 BWANA akaghairi katika jambo hili. Jambo hili halitakuwa, asema BWANA.

Mwanzo 9 : 16
16 Basi huo upinde utakuwa winguni; nami nitauangalia nipate kulikumbuka agano la milele lililoko kati ya Mungu na kila kiumbe hai katika wote wenye mwili kilichoko katika nchi.

Mwanzo 11 : 5
5 BWANA akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.

Mwanzo 11 : 7
7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.

Hesabu 11 : 25
25 Ndipo BWANA akashuka ndani ya wingu, akanena naye, akatwaa sehemu ya roho iliyokuwa juu ya Musa, akaitia juu ya wale wazee sabini; ikawa, roho hiyo ilipowashukia, wakatabiri, lakini hawakufanya hivyo tena.

Mwanzo 18 : 19
19 Kwa maana nimemchagua[6] ili awaamuru wanawe na vizazi vyake baada yake wadumishe njia ya BWANA, kwa kuwa wenye haki na kweli, ili BWANA naye akamtimizie Abrahamu ahadi zake.

Mwanzo 18 : 21
21 basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.

Mwanzo 18 : 33
33 Basi BWANA alipokwisha kuzungumza na Abrahamu, akaenda zake; Abrahamu naye akarudi mahali pake.

Mwanzo 19 : 29
29 Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Abrahamu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu.

Mwanzo 22 : 12
12 Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, kwa kuwa hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.

Mwanzo 28 : 13
13 ⑩ Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Abrahamu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii unayolala nitakupa wewe na uzao wako.

Mwanzo 35 : 13
13 ⑯ Mungu akakwea juu kutoka kwake mahali hapo aliposema naye.

Kutoka 2 : 24
24 ② Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Abrahamu na Isaka na Yakobo.

Kutoka 3 : 8
8 ⑫ nami nimeshuka ili niwaokoe kutoka kwa mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hadi nchi njema, kisha pana; nchi itiririkayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *