Biblia inasema nini kuhusu Amri – Mistari yote ya Biblia kuhusu Amri

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Amri

Kutoka 13 : 10
10 Kwa hiyo utaitunza amri hii kwa wakati wake mwaka baada ya mwaka.

Kutoka 20 : 17
17 Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala chochote alicho nacho jirani yako.

Kumbukumbu la Torati 5 : 21
21 ⑬ Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng’ombe wake, wala punda wake, wala kitu chochote alicho nacho jirani yako.

Kumbukumbu la Torati 4 : 5
5 Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama BWANA, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki.

Kumbukumbu la Torati 4 : 10
10 ⑪ siku ile uliyosimama mbele za BWANA wako huko Horebu, BWANA aliponiambia, Nikusanyieni watu hawa, nami nitawafanya wasikilize maneno yangu, ili wajifunze kunicha mimi siku zote watakazoishi duniani, wakapate na kuwafundisha watoto wao.

Kumbukumbu la Torati 6 : 9
9 Tena yaandike juu ya miimo ya nyumba yako, na juu ya malango yako.

Kumbukumbu la Torati 11 : 21
21 ili siku zenu zifanywe nyingi, na za vijana vyenu nao, juu ya nchi BWANA aliyowaapia baba zenu kuwa atawapa, kama zilivyo siku za mbingu juu ya nchi.

Kumbukumbu la Torati 32 : 47
47 ⑧ Kwa maana si jambo lisilofaa kwenu; maana, ni maisha yenu, na kwa jambo hili mtazifanya siku zenu kuwa nyingi juu ya nchi mwivukiayo Yordani kuimiliki.

Yoshua 8 : 35
35 ④ Hapakuwa na hata neno moja katika hayo aliyoamuru Musa, ambalo Yoshua hakulisoma mbele ya kusanyiko lote la Waisraeli, na mbele ya wanawake, na watoto, na wageni waliokaa nao.

2 Mambo ya Nyakati 17 : 9
9 ⑩ Wakafundisha katika Yuda, wenye kitabu cha Torati ya BWANA; wakazunguka katika miji yote ya Yuda, wakafundisha kati ya watu.

Nehemia 8 : 8
8 Nao wakasoma katika kitabu, katika Torati ya Mungu, kwa sauti ya kusikika; wakaeleza maana yake, hata wakayafahamu yaliyosomwa.

Zaburi 78 : 7
7 Wamwekee Mungu tumaini lao. Wala wasiyasahau matendo ya Mungu, Bali wazishike amri zake.

Mithali 3 : 4
4 ② Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele za Mungu na mbele ya mwanadamu.

Mithali 6 : 21
21 Yafunge hayo katika moyo wako daima; Jivike hayo shingoni mwako.

Mithali 7 : 4
4 Mwambie hekima, Wewe ndiwe dada yangu; Mwite ufahamu jamaa yako mwandani.

Isaya 57 : 8
8 Na nyuma ya milango na miimo umeweka kumbukumbu lako; kwa maana umejifunua nafsi yako kwa ajili ya mwingine, si kwa ajili yangu, ukakwea juu; umekipanua kitanda chako, nawe umefanya maagano na hao; ulikipenda kitanda chao hapo ulipokiona.

Yeremia 11 : 4
4 Niliyowaamuru baba zenu, siku ile nilipowatoa katika nchi ya Misri, katika tanuri ya chuma, nikisema, Itiini sauti yangu, mkafanye sawasawa na yote niwaagizayo ninyi; ndivyo mtakavyokuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu;

Zekaria 7 : 10
10 tena msimdhulumu mjane, wala yatima, wala mgeni, wala maskini; wala mtu awaye yote miongoni mwenu asiwaze mabaya juu ya ndugu yake moyoni mwake.

Zekaria 8 : 17
17 ③ wala mtu wa kwenu asiwaze mabaya moyoni mwake juu ya jirani yake; wala msipende kiapo cha uongo; maana hayo yote ndiyo niyachukiayo, asema BWANA.

Mathayo 5 : 16
16 ⑥ Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.

Mathayo 5 : 24
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.

Mathayo 5 : 48
48 Basi ninyi iweni wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Luka 6 : 36
36 Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.

Mathayo 6 : 4
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Mathayo 6 : 8
8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *