Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Amramu
Kutoka 6 : 18
18 Na wana wa Kohathi; ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli; na miaka ya maisha ya huyo Kohathi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na mitatu.
Kutoka 6 : 20
20 Huyo Amramu akamwoa Yokebedi shangazi yake; naye akamzalia Haruni, na Musa; na miaka ya maisha yake Amramu ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba.
Hesabu 26 : 59
59 Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi, binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amramu Haruni, na Musa, na Miriamu dada yao.
1 Mambo ya Nyakati 6 : 3
3 ⑬ Na wana wa Amramu; Haruni, na Musa, na Miriamu. Na wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.
1 Mambo ya Nyakati 6 : 18
18 Na wana wa Kohathi walikuwa Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.
1 Mambo ya Nyakati 23 : 13
13 Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za BWANA, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.
Hesabu 3 : 19
19 Na wana wa Kohathi kwa jamaa zao ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.
Hesabu 3 : 27
27 Na katika Kohathi ni jamaa ya Waamrami, na jamaa ya Waishari, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya hao Wauzieli; hizo ni jamaa za Wakohathi.
1 Mambo ya Nyakati 26 : 23
23 ⑱ Wa Waamrami wa Waishari, wa Wahebroni, wa Wauzieli;
Kutoka 6 : 20
20 Huyo Amramu akamwoa Yokebedi shangazi yake; naye akamzalia Haruni, na Musa; na miaka ya maisha yake Amramu ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba.
Ezra 10 : 34
34 Na wa wazawa wa Bani; Maadai, na Amramu, na Ueli,
1 Mambo ya Nyakati 1 : 41
41 Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani.
Leave a Reply