Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Amani
Mwanzo 13 : 9
9 ⑦ Je! Nchi hii yote haiko mbele yako? Basi jitenge nami, nakusihi; ukienda upande wa kushoto, nitakwenda upande wa kulia; ukienda upande wa kulia, nitakwenda upande wa kushoto.
Mwanzo 26 : 29
29 ⑧ ya kuwa hutatutenda mabaya, iwapo sisi hatukukugusa wewe, wala hatukukutendea ila mema, tukakuacha uende zako kwa amani; nawe sasa u mbarikiwa wa BWANA.
Esta 10 : 3
3 Kwa maana Mordekai Myahudi akiwa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwajali watu wake, na kuiangalia hali njema ya wazawa wao wote.
Mwanzo 45 : 24
24 Akaagana na ndugu zake, wakaenda zao; naye akawaambia, Msigombane njiani.
Mambo ya Walawi 26 : 6
6 Nami nitawapa amani katika nchi, tena mtalala na hakuna atakayewatia hofu; nami nitawakomesha wanyama wabaya katika nchi yenu, wala hautapita upanga katika nchi yenu.
Ayubu 5 : 24
24 Nawe utajua ya kwamba hema yako ni salama; Na zizi lako utalikagua, wala usikose kitu.
Zaburi 34 : 14
14 Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.
Zaburi 120 : 7
7 Mimi nazingatia amani; Bali ninenapo, wao wanataka vita.
Zaburi 133 : 1
1 Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza, Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja.
Mithali 12 : 20
20 Hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu; Bali wafanyao mashauri ya amani, kwao kuna furaha.
Mithali 15 : 17
17 Chakula cha mboga palipo na upendo; Ni bora kuliko ng’ombe aliyenona pamoja na kuchukiana.
Mithali 16 : 7
7 ⑫ Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye.
Mithali 17 : 1
1 Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.
Mithali 17 : 14
14 Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji; Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.
Mithali 20 : 3
3 ④ Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana.
Mhubiri 4 : 6
6 Heri konzi moja pamoja na utulivu, Kuliko konzi mbili pamoja na taabu; na kufukuza upepo.
Isaya 2 : 4
4 Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.
Isaya 45 : 7
7 Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni BWANA, niyatendaye hayo yote.
Yeremia 29 : 7
7 ③ Kautakieni amani mji ule, ambao nimewafanya mchukuliwe mateka, mkauombee kwa BWANA; kwa maana katika amani yake mji huo ninyi mtapata amani.
Hosea 2 : 18
18 Nami siku hiyo nitafanya agano na wanyama wa mashamba kwa ajili yao, tena na ndege wa angani, tena na wadudu wa nchi; nami nitavivunja upinde na upanga na silaha vitoke katika nchi, nami nitawalalisha salama salimini.
Zekaria 8 : 19
19 ④ BWANA wa majeshi asema hivi, Saumu ya mwezi wa nne, na saumu ya mwezi wa tano, na saumu ya mwezi wa saba, na saumu ya mwezi wa kumi, zitakuwa furaha na shangwe, na sikukuu za kuchangamkia, kwa nyumba ya Yuda; basi zipendeni kweli na amani.
Leave a Reply