Biblia inasema nini kuhusu Alfa – Mistari yote ya Biblia kuhusu Alfa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Alfa

Ufunuo 1 : 8
8 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, asema Bwana Mungu, aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi.

Ufunuo 1 : 11
11 ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika kitabu, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.

Ufunuo 21 : 6
6 ④ Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye aliye na kiu, maji kutoka chemchemi ya maji ya uzima, bure.

Ufunuo 22 : 13
13 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.

Isaya 41 : 4
4 Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, BWANA, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye.

Isaya 44 : 6
6 ① BWANA, Mfalme wa Israeli, Mkombozi wako, BWANA wa majeshi, asema hivi; Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho; zaidi yangu mimi hapana Mungu.

Isaya 48 : 12
12 ⑱ Nisikilize mimi, Ee Yakobo; na Israeli, niliyekuita; mimi ndiye. Mimi ni wa kwanza, na mimi ni wa mwisho pia.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *