Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Alama
Kumbukumbu la Torati 19 : 14
14 Usiiondoe alama ya mpaka wa jirani yako, waliouweka watu wa kale katika urithi wako, utakaorithi ndani ya nchi akupayo BWANA, Mungu wako, uimiliki.
Kumbukumbu la Torati 27 : 17
17 ⑩ Na alaaniwe aondoaye mpaka wa jirani yake. Na watu wote waseme, Amina.
Ayubu 24 : 2
2 Wako waziondoao alama za mipaka; Huyachukua makundi na kuyalisha.
Mithali 22 : 28
28 Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani, Uliowekwa na baba zako.
Mithali 23 : 10
10 Usiiondoe alama ya mpaka wa zamani; Wala usiingie katika mashamba ya yatima;
Hosea 5 : 10
10 ⑪ Wakuu wa Yuda ni kama watu waondoao alama ya mpaka; nitawamwagia ghadhabu yangu kama maji.
Leave a Reply