Biblia inasema nini kuhusu Ahazi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Ahazi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ahazi

2 Wafalme 15 : 38
38 Yothamu akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi baba yake. Na Ahazi mwanawe akatawala mahali pake.

2 Wafalme 16 : 1
1 Katika mwaka wa kumi na saba wa Peka mwana wa Remalia Ahazi mwana wa Yothamu mfalme wa Yuda alianza kutawala.

2 Mambo ya Nyakati 27 : 9
9 Yothamu akalala na babaze, wakamzika katika mji wa Daudi; na Ahazi mwanawe akatawala mahali pake.

2 Mambo ya Nyakati 28 : 1
1 ⑲ Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; akatawala katika Yerusalemu miaka kumi na sita; wala hakufanya yaliyo ya adili machoni pa BWANA, kama Daudi babaye;

2 Wafalme 16 : 4
4 Kisha akatoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti mbichi.

2 Mambo ya Nyakati 28 : 4
4 Akatoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu, na vilimani, na chini ya kila mti wenye majani mabichi.

2 Mambo ya Nyakati 28 : 25
25 Na katika kila mji wa Yuda akafanya mahali pa juu pa kuifukizia miungu mingine uvumba, akamkasirisha BWANA, Mungu wa babaze.

2 Wafalme 16 : 6
6 ② Wakati huo Resini mfalme wa Shamu akawarudishia Washami Elathi, akawafukuza Wayahudi kutoka Elathi; nao Washami wakaja Elathi, wakakaa humo hata leo.

2 Mambo ya Nyakati 28 : 8
8 Waisraeli wakachukua mateka ndugu zao wafungwa elfu mia mbili wakiwemo wanawake, watoto wa kiume na kike, pia wakachukua kwao nyara nyingi, wakazileta nyara Samaria.

2 Wafalme 16 : 9
9 ⑤ Na huyo mfalme wa Ashuru akamsikia; mfalme wa Ashuru akapanda juu ya Dameski, akautwaa, akawahamisha watu wake mateka mpaka Kiri, akamwua Resini.

2 Wafalme 16 : 18
18 Na ukumbi wa sabato walioujenga katika hiyo nyumba, na mahali pa kuingia pake mfalme palipokuwapo nje, akavigeuza kuikabili nyumba ya BWANA, kwa sababu ya mfalme wa Ashuru.

2 Mambo ya Nyakati 28 : 21
21 Kwa maana Ahazi alitwaa sehemu katika nyumba ya BWANA, na katika nyumba ya mfalme, na ya wakuu, akampa mfalme wa Ashuru; asisaidiwe na jambo hilo.

2 Wafalme 16 : 16
16 Akafanya hivyo Uria kuhani, sawasawa na yote aliyoyaamuru mfalme Ahazi.

2 Wafalme 20 : 11
11 ⑩ Isaya nabii akamlilia BWANA; akakirudisha nyuma kile kivuli madaraja kumi, ambayo kilikuwa kimeshuka katika madaraja ya Ahazi.

Isaya 38 : 8
8 Tazama, nitakirudisha nyuma kivuli madaraja kumi, ambayo kilishuka juu ya duara ya Ahazi kwa sababu ya jua. Basi jua likarudi madaraja kumi katika hiyo duara, ambayo limekwisha kushuka.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *