Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia agano na macho yangu
Ayubu 31 : 1
1 Nilifanya agano na macho yangu; Basi ningewezaje kumwangalia msichana?
Ayubu 31 : 1 – 40
1 Nilifanya agano na macho yangu; Basi ningewezaje kumwangalia msichana?
2 Kwani sehemu ya Mungu itokayo juu ingekuwa nini, Na urithi wa Mwenyezi utokao juu?
3 Je! Siyo msiba kwa wasio haki, Na hasara kwao watendao uovu?
4 Je! Yeye hazioni njia zangu, Na kuzihesabu hatua zangu zote?
5 Kwamba nimetembea katika ubatili, Na mguu wangu umeukimbilia udanganyifu;
6 (Na nipimwe katika mizani iliyo sawasawa, Ili Mungu aujue uelekevu wangu);
7 Kwamba hatua yangu imekengeuka na kuiacha njia, Na moyo wangu kuyaandama macho yangu, Tena kwamba kipaku chochote kimeshikamana na mikono yangu;
8 Basi na nipande, mwingine ale; Naam, mazao ya shamba langu na yang’olewe.
9 Kama moyo wangu ulishawishwa kwa mwanamke, Nami nimeotea mlangoni pa jirani yangu;
10 Ndipo hapo mke wangu na asage kwa mwingine, Na wengine na wainame juu yake.
11 Kwani hilo lingekuwa kosa kuu; Naam, lingekuwa ni uovu wa kuadhibiwa na waamuzi;
12 Kwa kuwa ni moto uteketezao hata Uharibifu, Nao ungeyang’oa mavuno yangu yote.
13 Kama nimeidharau kesi ya mtumishi wangu, au ya kijakazi changu, Waliposhindana nami;
14 Basi Mungu atakapoinuka nitafanya nini? Naye atakapozuru, nitamjibuje?
15 Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye? Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni?
16 Ikiwa nimewanyima maskini haja zao, Au kama nimeyatia kiwi macho ya mwanamke mjane;
17 Au kama nimekula tonge langu peke yangu, Mayatima wasipate kulila;
18 (La, tangu ujana wangu alikuwa pamoja nami kama kwa baba; Nami nimekuwa ni kiongozi wa mjane tangu tumbo la mamangu);
19 Ikiwa nimemwona mtu kuangamia kwa kukosa nguo, Au wahitaji kukosa mavazi;
20 Ikiwa viuno vyake havikunibariki, Au kama hakupata moto kwa manyoya ya kondoo wangu;
21 Ikiwa nimewainulia mayatima mkono, Nilipoona msaada wangu langoni;
22 Basi bega langu na lianguke kutoka mahali pake, Na mkono wangu uvunjike mfupani mwake.
23 Kwani msiba utokao kwa Mungu ulikuwa na kitisho kwangu, Na kwa sababu ya ukuu wake sikuweza kufanya neno.
24 Ikiwa nimeifanya dhahabu kuwa tumaini langu, Na kuiambia dhahabu safi, Wewe u tegemeo langu;
25 Kama nilifurahi kwa kuwa mali yangu ilikuwa nyingi, Na kwa sababu mkono wangu umepata vitu vingi;
26 Kama nililitazama jua lilipoangaza, Au mwezi ukiendelea kung’aa;
27 Na moyo wangu umeshawishwa kwa siri, Na midomo yangu imeubusu mkono wangu;
28 Hilo nalo lingekuwa uovu wa kuadhibiwa na waamuzi; Kwani ningemwambia uongo Mungu aliye juu.
29 Kama nilifurahi kwa kuangamia kwake huyo aliyenichukia, Au kujitukuza alipopatikana na maovu;
30 (Naam, sikukiacha kinywa changu kufanya dhambi Kwa kuutaka uhai wake kwa kuapiza);
31 Kama watu wa hemani mwangu hawakunena, Ni nani awezaye kumpata mtu asiyeshibishwa na yeye kwa nyama?
32 Mgeni hakulala njiani; Lakini nilimfungulia msafiri milango yangu;
33 Ikiwa kama mwanadamu nimeyafunika makosa yangu, Kwa kuuficha uovu wangu kifuani mwangu;
34 Kwa sababu niliwaogopa mkutano mkubwa, Na dharau la jamaa lilinitia hofu, Hata nilinyamaa kimya, nisitoke mlangoni.
35 Laiti ningekuwa na mtu wa kunisikia! (Tazama, sahihi yangu ni hii, Mwenyezi na anijibu); Laiti ningekuwa na hayo mashitaka yaliyoandikwa na adui yangu!
36 Hakika ningeyachukua mabegani; Ningejifunga mfano wa kilemba.
37 Ningemwambia hesabu ya hatua zangu Ningemkaribia kama vile mkuu.
38 Kama nchi yangu imelia juu yangu, Na matuta yake hulia pamoja;
39 Kama nimeyala matunda yake pasipo kulipa, Au kama nimewafanya wenyewe kupotewa na uhai;
40 Miiba na imee badala ya ngano, Na magugu badala ya shayiri. Maneno ya Ayubu yamekoma hapa.
Mathayo 5 : 28
28 ⑯ lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
Wafilipi 4 : 8
8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.
Wagalatia 5 : 1
1 Katika uhuru huo Kristo alituweka huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.
Leave a Reply