Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Agano
Yoshua 9 : 21
21 ⑳ Wakuu waliwaambia, Waacheni wawe hai; basi wakawa wenye kupasua kuni, na wenye kuteka maji, kwa ajili ya mkutano wote; vile vile kama hao wakuu walivyowaambia.
Wagalatia 3 : 15
15 Ndugu zangu, nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna mtu alibatilishaye, wala kuliongeza neno.
Yoshua 9 : 20
20 ⑲ Tutawafanyia neno hili, kisha tutawaacha wawe hai; hasira isije juu yetu, kwa ajili ya hicho kiapo tulichowaapia.
Yeremia 34 : 21
21 ③ Na Sedekia, mfalme wa Yuda, na wakuu wake nitawatia katika mikono ya adui zao, na katika mikono ya watu wale wanaowatafuta roho zao, na katika mikono ya jeshi la mfalme wa Babeli, waliokwenda zao na kuwaacheni.
Ezekieli 17 : 18
18 Kwa maana amekidharau kiapo kwa kulivunja agano; na tazama, ametia mkono wake, na pamoja na hayo ameyatenda mambo hayo yote; hataokoka.
Wagalatia 3 : 15
15 Ndugu zangu, nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano la mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna mtu alibatilishaye, wala kuliongeza neno.
Kumbukumbu la Torati 29 : 15
15 ila na yeye aliyesimama hapa nasi hivi leo mbele ya BWANA, Mungu wetu, na yeye naye asiyekuwapo pamoja nasi leo;
Kutoka 24 : 8
8 ⑰ Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, Hii ndiyo damu ya agano alilolifanya BWANA pamoja nanyi katika maneno haya yote.
Kutoka 24 : 7
7 Kisha akakitwaa Kitabu cha Agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena BWANA tutayatenda, nasi tutatii.
2 Samweli 21 : 6
6 basi, na tutolewe watu saba katika wanawe, nasi tutawatundika mbele za BWANA katika Gibeoni, katika mlima wa BWANA. Mfalme akasema, Nitawatoa.
Yeremia 34 : 22
22 ④ Tazama, nitawapa amri yangu, asema BWANA, na kuwarejesha kwenye mji huu; nao watapigana nao, na kuutwaa, na kuuteketeza kwa moto; nami nitaifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, isikaliwe na mtu.
Ezra 10 : 19
19 ⑯ Nao wakatoa ahadi ya kwamba wataachana na wake zao; na kwa kuwa walikuwa na hatia, wakatoa kondoo dume kwa hatia yao.
Maombolezo 5 : 1 – 232
1 Ee BWANA, kumbuka yaliyotupata; Utazame na kuiona aibu yetu.
2 Urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni; Na nyumba zetu kuwa mali ya mataifa.
3 Tumekuwa yatima waliofiwa na baba; Mama zetu wamekuwa kama wajane.
4 Tumekunywa maji yetu kwa fedha; Kuni zetu twauziwa.
5 Watufuatiao wako juu ya shingo zetu; Tumechoka, tusipate pumziko lolote.
6 Tumewapa hao Wamisri mkono; Na Waashuri nao, ili tushibe chakula.
7 Baba zetu walitenda dhambi hata hawako; Na sisi tumeyachukua maovu yao.
8 Watumwa wanatutawala; Hakuna mtu wa kutuokoa na mikono yao.
9 Twapata chakula kwa kujihatarisha nafsi zetu; Kwa sababu ya upanga wa nyikani.
10 Ngozi yetu ni nyeusi kama tanuri; Kwa sababu ya joto ya njaa ituteketezayo.
11 Wanawake katika Sayuni wanashikwa kwa nguvu; Na mabikira katika miji ya Yuda.
12 Wakuu hutundikwa kwa mikono yao; Nyuso za wazee hazipewi heshima.
13 Vijana huyachukua mawe ya kusagia; Na watoto hujikwaa chini ya kuni.
14 Wazee wameacha kwenda langoni; Na vijana kwenda ngomani.
15 Furaha ya mioyo yetu imekoma; Machezo yetu yamegeuka maombolezo.
16 Taji ya kichwa chetu imeanguka; Ole wetu! Kwa kuwa tumetenda dhambi.
17 Kwa sababu hiyo mioyo yetu imezimia; Kwa ajili ya hayo macho yetu hayaoni vema.
18 Kwa ajili ya mlima Sayuni ulio ukiwa, Mbweha hutembea juu yake.
19 Wewe, BWANA, unadumu milele; Kiti chako cha enzi ni tangu kizazi hata kizazi.
20 Mbona watusahau sikuzote; Na kutuacha muda huu mwingi?
21 Ee BWANA, utugeuze kwako, nasi tutageuka; Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale.
22 Ingawa wewe umetukataa kabisa; Nawe una hasira nyingi sana juu yetu.
Leave a Reply