Biblia inasema nini kuhusu agano – Mistari yote ya Biblia kuhusu agano

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia agano

Zaburi 105 : 8 – 11
8 Analikumbuka agano lake milele; Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
9 Agano alilofanya na Abrahamu, Na ahadi yake kwa Isaka.
10 Alilomthibitishia Yakobo liwe amri, Na Israeli liwe agano la milele.
11 Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Kama fungu la urithi wenu.

Zaburi 74 : 20
20 Ulitafakari agano lako; Maana mahali kwenye giza katika nchi Kumejaa makao ya ukatili.

Zaburi 105 : 8
8 Analikumbuka agano lake milele; Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.

Nehemia 9 : 38
38 Na kwa sababu ya hayo yote sisi tunafanya agano la hakika, na kuliandika; na wakuu wetu, na Walawi wetu, na makuhani wetu, wanalitilia mhuri.

Yeremia 31 : 31 – 34
31 ⑬ Angalia, siku zinakuja, asema BWANA, nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
32 ⑭ Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nilikuwa mume kwao, asema BWANA.
33 ⑮ Bali agano hili ndilo nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
34 ⑯ Wala hawatamfundisha kila mtu jirani yake, na kila mtu ndugu yake, wakisema, Mjue BWANA; kwa maana watanijua wote, tangu mtu aliye mdogo miongoni mwao hadi aliye mkubwa miongoni mwao, asema BWANA; maana nitausamehe uovu wao, wala dhambi yao sitaikumbuka tena.

Warumi 9 : 7 – 13
7 ③ Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazawa wa Abrahamu, bali, Katika Isaka wazawa wako wataitwa;
8 ④ yaani, si watoto wa mwili walio watoto wa Mungu, bali watoto wa ile ahadi wanahesabiwa kuwa wazawa.
9 ⑤ Kwa maana neno la ahadi ni hili, Panapo wakati huu nitakuja, na Sara atapata mtoto wa kiume.
10 ⑥ Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu,
11 (kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye),
12 ⑦ aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo.
13 ⑧ Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.

Waraka kwa Waebrania 6 : 18
18 ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *