Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia afya
1 Wakorintho 6 : 19 – 20
19 ⑲ Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;
20 ⑳ maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
Mithali 17 : 22
22 Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; Bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.
1 Wakorintho 3 : 17
17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi.
3 Yohana 1 : 2
2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
Mithali 16 : 24
24 Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani.
1 Wakorintho 10 : 31
31 ② Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.
Mithali 4 : 20 – 22
20 Mwanangu, sikiliza maneno yangu; Tega sikio lako, uzisikie kauli zangu.
21 Zisiondoke machoni pako; Uzihifadhi ndani ya moyo wako.
22 Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote.
1 Wakorintho 3 : 16
16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
1 Petro 2 : 24
24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.
1 Timotheo 4 : 7 – 8
7 ⑮ Bali hadithi za kale, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.
8 ⑯ Maana, mazoezi ya viungo vya mwili yana manufaa kidogo, lakini utauwa una manufaa ya kila aina; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.
Mambo ya Walawi 19 : 28
28 Msichanje chale yoyote katika nyama ya miili yenu kwa ajili ya wafu, wala msiandike alama miilini mwenu; mimi ndimi BWANA.
Leave a Reply