Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Afeki
Yoshua 19 : 30
30 na Uma pia, na Afeka, na Rehobu; miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.
Waamuzi 1 : 31
31 Asheri naye hakuwatoa wenyeji wa Aka, wala hao waliokaa Sidoni, wala hao wa Alabu, wala hao wa Akzibu, wala hao wa Helba, wala hao wa Afeka, wala hao wa Rehobu;
1 Samweli 4 : 11
11 Hilo sanduku la Mungu likatwaliwa; na Hofni na Finehasi, wale wana wawili wa Eli, wakauawa.
1 Samweli 29 : 1
1 ⑩ Basi hao Wafilisti wakakusanya majeshi yao yote huko Afeki; nao Waisraeli wakafanya kambi karibu na chemchemi iliyoko Yezreeli.
1 Samweli 31 : 13
13 ① Kisha wakaitwaa mifupa yao, na kuizika chini ya mkwaju huko Yabeshi, nao wakafunga siku saba.
Yoshua 12 : 18
18 mfalme wa Afeka, mmoja; na mfalme wa Lasharoni, mmoja;
1 Wafalme 20 : 30
30 Lakini waliosalia wakakimbia mpaka Afeki, mjini; na ukuta ukaanguka juu ya watu elfu ishirini na saba waliosalia. Ben-hadadi naye akakimbia, akaingia mjini, katika chumba cha ndani.
Leave a Reply