Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Adui
Kutoka 23 : 5
5 Ukimwona punda wake huyo akuchukiaye akiwa ameanguka chini ya mzigo wake, na wewe ungejizuia usimsaidie, lazima umsaidie.
Ayubu 31 : 30
30 (Naam, sikukiacha kinywa changu kufanya dhambi Kwa kuutaka uhai wake kwa kuapiza);
Zaburi 35 : 28
28 Na ulimi wangu utanena haki yako, Na sifa zako mchana kutwa.
Mithali 24 : 18
18 BWANA asije akaliona hilo, likamkasirisha; Akageuzia mbali naye hasira yake.
Mithali 25 : 22
22 ⑳ Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu.
Mathayo 5 : 48
48 Basi ninyi iweni wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Luka 6 : 36
36 Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
Warumi 12 : 14
14 Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.
Warumi 12 : 20
20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
Zaburi 56 : 5
5 Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu, Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.
Zaburi 57 : 4
4 Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.
Zaburi 57 : 6
6 Wameweka wavu ili kuninasa miguu; Nimevunjika moyo; Wamechimba shimo njiani mwangu; Lakini wao wenyewe wametumbukia humo!
Zaburi 62 : 4
4 Mpango wao ni kumwangusha tu mtu mwenye cheo; Huufurahia uongo. Kwa kinywa chao hubariki; Kwa moyo wao hulaani.
Zaburi 69 : 4
4 Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali ni wengi, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nililipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.
Zaburi 69 : 9
9 Maana mvuto wa nyumba yako umenila, Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.
Zaburi 71 : 10
10 ⑥ Kwa maana adui zangu wananiamba, Nao wanaotaka kuniua hushauriana.
Zaburi 102 : 8
8 Adui zangu wananilaumu mchana kutwa; Wanaonichukia kana kwamba wana wazimu Wakitaja jina langu katika laana zao.
Zaburi 109 : 5
5 Wamenilipa mabaya kwa mema yangu, Na chuki badala ya upendo wangu.
2 Samweli 19 : 6
6 kwa kuwa unawapenda wakuchukiao, na unawachukia wakupendao. Maana umetangaza leo ya kuwa wakuu na watumishi wako si kitu kwako; maana leo nimetambua hivi; kama Absalomu angalikuwa hai, na sisi sote tungalikuwa wafu leo, ingekuwa vyema machoni pako.
2 Samweli 19 : 13
13 Kisha mkamwambie Amasa, Je! Si wewe uliye mfupa wangu, na nyama yangu? Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, usipokuwa wewe jemadari wa jeshi mbele yangu daima mahali pa Yoabu.
Leave a Reply