Biblia inasema nini kuhusu adhabu ya wizi – Mistari yote ya Biblia kuhusu adhabu ya wizi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia adhabu ya wizi

Mambo ya Walawi 6 : 1 – 5
1 BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2 Mtu awaye yote akifanya dhambi, na kuasi juu ya BWANA, akamdanganya mwenziwe katika jambo la amana, au la mapatano, au la kunyang’anya, au kumwonea mwenziwe;
3 au kupata kitu kilichopotea na kutenda la uongo juu yake, na kuapa kwa uongo; katika mambo hayo yote mojawapo atakalolitenda mtu, na kufanya dhambi kwalo;
4 ndipo itakapokuwa, akiwa amefanya dhambi, na kupata hatia, atarudisha hicho alichokipata kwa kunyang’anya, au kitu kile alichokipata kwa kuonea, au ile amana aliyowekewa, au kitu kile kilichopotea alichokipata yeye,
5 au kitu chochote ambacho amekiapia uongo; atakirudisha hata kwa utimilifu wake, kisha ataongeza na sehemu ya tano zaidi juu yake; naye atampa huyo mwenyewe, siku hiyo ambayo atakapohukumiwa kuwa mwenye hatia.

Kutoka 22 : 1
1 ⑪ Mtu akiiba ng’ombe au kondoo, na kumchinja, au kumwuza; atalipa ng’ombe watano badala ya ng’ombe mmoja, na kondoo wanne badala ya kondoo mmoja.

Kutoka 21 : 16
16 Yeye amwibaye mtu, na kumwuza, au akipatikana mkononi mwake, sharti atauawa huyo.

Kutoka 21 : 24
24 ⑤ jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu,

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *