Biblia inasema nini kuhusu Adhabu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Adhabu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Adhabu

Hesabu 35 : 31
31 Tena, msipokee fidia kwa ajili ya uhai wa mwuaji, ambaye amekuwa na hatia ya mauti; Lakini lazima atauawa.

Mwanzo 9 : 6
6 Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu, maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.

Hesabu 35 : 21
21 au akampiga kwa mkono wake kwa kuwa ni adui, naye akafa; yeye aliyempiga lazima atauawa; yeye ni mwuaji; mwenye kutwaa kisasi cha damu atamwua mwuaji, hapo atakapokutana naye.

Hesabu 35 : 33
33 ③ Hivi hamtaitia unajisi nchi ambayo mwakaa; kwa kuwa damu huitia nchi unajisi; wala hapana sadaka itoshayo kwa ajili ya nchi, kwa ajili ya damu iliyomwagwa ndani yake, isipokuwa ni damu ya huyo aliyeimwaga.

Kumbukumbu la Torati 17 : 6
6 Huyo atakayeuawa na auawe kwa midomo ya mashahidi wawili, au mashahidi watatu; asiuawe kwa mdomo wa shahidi mmoja. Ebr 10:28

Mambo ya Walawi 20 : 10
10 Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mwanamume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.

Kumbukumbu la Torati 22 : 24
24 watoeni nje katika lango la mji ule, mkawapige kwa mawe hata wafe; yule kijana, kwa kuwa hakupiga ukelele, naye yu ndani ya mji; na yule mume, kwa kuwa amemtweza mke wa mwenzake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Mambo ya Walawi 20 : 12
12 Na mwanamume akilala na mkwewe mwanamke, wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo upotovu; damu yao itakuwa juu yao.

Mambo ya Walawi 20 : 14
14 ② Tena mwanamume akimwoa mke pamoja na mama yake, ni uovu mkuu; watachomwa moto, yeye mume na hao wanawake pia; ili kwamba usiwe uovu kati yenu.

Kutoka 22 : 19
19 Mtu yeyote alalaye na mnyama sharti atauawa.

Mambo ya Walawi 20 : 16
16 Tena mwanamke akimmwendea mnyama yeyote, na kulala pamoja naye, mtamwua huyo mwanamke, na mnyama pia; hakika watauawa; damu yao itakuwa ni juu yao.

Mambo ya Walawi 18 : 22
22 ⑤ Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.

Mambo ya Walawi 20 : 13
13 ① Tena mwanamume akilala pamoja na mwanamume, kama alalavyo na mwanamke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.

Kumbukumbu la Torati 22 : 24
24 watoeni nje katika lango la mji ule, mkawapige kwa mawe hata wafe; yule kijana, kwa kuwa hakupiga ukelele, naye yu ndani ya mji; na yule mume, kwa kuwa amemtweza mke wa mwenzake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Kumbukumbu la Torati 22 : 25
25 Lakini yule mtu mume kama akimkuta kondeni binti aliyeposwa, naye mume akamtenza nguvu, akalala naye; yule mtu mume aliyelala naye na afe pekee;

Zekaria 5 : 4
4 ⑳ Nitaituma itokee, asema BWANA wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi, na katika nyumba ya yeyote aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katika nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.

Kutoka 21 : 16
16 Yeye amwibaye mtu, na kumwuza, au akipatikana mkononi mwake, sharti atauawa huyo.

Kumbukumbu la Torati 24 : 7
7 ⑥ Mtu akionekana anamwiba nduguze mmojawapo katika wana wa Israeli, akamfanya kama mtumwa, au kumwuza; na afe mwizi huyo; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *