Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Achori
Yoshua 7 : 26
26 Kisha wakakusanya juu yake rundo kubwa la mawe hata leo; naye BWANA akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori,[3] hata leo.
Yoshua 15 : 7
7 kisha mpaka ukaendelea hadi Debiri kutoka bonde la Akori, na ukaendelea upande wa kaskazini, kwa kuelekea Gilgali, iliyo mkabala wa kukwelea kwenda Adumimu, ulio upande wa kusini wa mto; kisha huo mpaka ukaendelea hadi kufika kwenye maji ya Enshemeshi, na kuishia Enrogeli;
Isaya 65 : 10
10 Na Sharoni itakuwa zizi la makundi ya kondoo, na bonde la Akori mahali pa kulala makundi ya ng’ombe, kwa ajili ya watu wangu walionitafuta.
Hosea 2 : 15
15 Nami nitampa mashamba yake ya mizabibu toka huko, na bonde la Akori kuwa mlango wa tumaini; naye ataniitikia huko, kama siku zile za ujana wake, na kama siku ile alipopanda kutoka nchi ya Misri.
Leave a Reply