Biblia inasema nini kuhusu Utiifu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Utiifu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Utiifu

Mwanzo 18 : 19
19 Kwa maana nimemchagua[6] ili awaamuru wanawe na vizazi vyake baada yake wadumishe njia ya BWANA, kwa kuwa wenye haki na kweli, ili BWANA naye akamtimizie Abrahamu ahadi zake.

Kutoka 19 : 5
5 Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,

Kutoka 20 : 6
6 ⑱ nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Kumbukumbu la Torati 5 : 10
10 ② nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Kutoka 24 : 7
7 Kisha akakitwaa Kitabu cha Agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, Hayo yote aliyoyanena BWANA tutayatenda, nasi tutatii.

Yoshua 24 : 24
24 Ndipo hao watu wakamwambia Yoshua, BWANA, Mungu wetu, ndiye tutakayemtumikia; na sauti yake ndiyo tutakayoitii.

Hesabu 9 : 23
23 bali lilipoinuliwa walisafiri. Kwa amri ya BWANA walipiga kambi yao, na kwa amri ya BWANA walisafiri; walimtii BWANA, kwa mkono wa Musa.

Hesabu 14 : 24
24 lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye amenifuata kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na wazao wake wataimiliki.

Yoshua 14 : 14
14 Kwa hiyo Hebroni ukawa urithi wa Kalebu, mwana wa Yefune, Mkenizi hata hivi leo, kwa sababu, alikuwa mwaminifu kwa BWANA, Mungu wa Israeli.

Yoshua 22 : 2
2 ⑩ naye akawaambia, Ninyi mmeyafuata hayo yote mliyoamriwa na Musa, mtumishi wa BWANA, nanyi mmeisikia sauti yangu katika yote niliyowaamuru mimi;

1 Wafalme 3 : 14
14 ④ Nawe ukienda katika njia zangu, na kuyashika mausia yangu, na amri zangu, kama baba yako Daudi alivyokwenda, basi nitazifanya siku zako kuwa nyingi.

2 Wafalme 18 : 6
6 Maana alishikamana na BWANA, hakuacha kumfuata, bali alizishika amri zake BWANA alizomwamuru Musa.

2 Wafalme 21 : 8
8 wala sitawapotosha Israeli miguu watoke katika nchi niliyowapa baba zao; wakiangalia tu na kufanya sawasawa na yote niliyowaamuru, na kwa kuishika torati yote aliyowaamuru mtumishi wangu Musa.

Nehemia 1 : 5
5 nikasema, Nakusihi, Ee BWANA, Mungu wa mbinguni, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, mwenye kutimiza agano lake na rehema zake kwa hao wampendao na kuzishika amri zake;

Zaburi 1 : 2
2 Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

Zaburi 18 : 44
44 Mara tu waliposikia habari zangu, wakanitii. Wageni walinijia wakinyenyekea.

Zaburi 25 : 10
10 Njia zote za BWANA ni fadhili na kweli, Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.

Zaburi 99 : 7
7 Akasema nao katika nguzo ya wingu. Wakashika shuhuda zake na amri aliyowapa.

Zaburi 103 : 18
18 ⑬ Kwa wale walishikao agano lake, Na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye.

Zaburi 103 : 21
21 ⑯ Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote, Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake.

Zaburi 111 : 10
10 ⑯ Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri, Sifa zake zadumu milele.

Zaburi 112 : 1
1 Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake.

Zaburi 119 : 2
2 Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote.

Zaburi 119 : 6
6 Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote.

Zaburi 119 : 8
8 Nitazitii amri zako, Usiniache kabisa.

Zaburi 119 : 10
10 Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako.

Zaburi 119 : 16
16 Nitajifurahisha sana kwa amri zako, Sitalisahau neno lako.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *