Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Upole
Zaburi 22 : 26
26 ⑰ Wapole watakula na kushiba, Wamtafutao BWANA watamsifu; Mioyo yenu na iishi milele.
Zaburi 25 : 9
9 Wenye upole atawaongoza katika haki, Wenye upole atawafundisha njia yake.
Zaburi 37 : 11
11 Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani.
Zaburi 76 : 9
9 Mungu aliposimama ili kuhukumu Na kuwaokoa wapole wa dunia wote pia.
Zaburi 147 : 6
6 BWANA huwategemeza wenye upole, Huwaangusha chini wenye jeuri.
Zaburi 149 : 4
4 Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake, Huwapamba wenye upole kwa wokovu.
Mithali 14 : 29
29 Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.
Mithali 15 : 1
1 Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.
Mithali 15 : 18
18 Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.
Mithali 16 : 32
32 Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.
Mithali 17 : 1
1 Afadhali mego kavu pamoja na utulivu, Kuliko nyumba yenye karamu nyingi pamoja na magomvi.
Mithali 19 : 11
11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake; Nayo ni fahari yake kusamehe makosa.
Mithali 20 : 3
3 ④ Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana.
Mithali 25 : 15
15 Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa; Na ulimi laini huvunja mfupa.
Mithali 29 : 8
8 Watu wenye dharau huwasha mji moto; Bali wenye hekima hugeuzia mbali ghadhabu.
Mhubiri 7 : 8
8 ① Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi.
Mhubiri 10 : 4
4 Roho yake mtawala ikiinuka kinyume chako, Usiondoke mara mahali pako ulipo; Kwa maana roho ya upole hutuliza machukizo yaliyo makubwa.
Isaya 11 : 4
4 bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.
Isaya 29 : 19
19 ⑮ Wanyenyekevu nao wataongeza furaha yao katika BWANA, na maskini katika wanadamu watafurahi katika Mtakatifu wa Israeli.
Maombolezo 3 : 30
30 Na amwelekezee yule ampigaye shavu lake; Ashibishwe mashutumu.
Amosi 3 : 3
3 Je! Watu wawili wanaweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?
Sefania 2 : 3
3 Mtafuteni BWANA, enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BWANA.
Mathayo 5 : 5
5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.
Mathayo 5 : 9
9 Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
Mathayo 5 : 42
42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.
Luka 6 : 29
29 Akupigaye shavu moja, mgeuzie la pili, naye akunyang’anyaye joho yako, usimzuilie na kanzu.
Mathayo 11 : 29
29 Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;
Mathayo 27 : 14
14 Asimjibu hata neno moja, hata mtawala akastaajabu sana.
Leave a Reply