Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Unyang’anyi
Zaburi 109 : 11
11 Mdai na anase vitu vyote alivyo navyo, Wageni na wateke mapato ya kazi yake.
Isaya 16 : 4
4 Watu wangu waliofukuzwa waache wakae pamoja nawe; katika habari za Moabu, uwe kimbilio kwake mbele ya uso wake anayeharibu; maana yeye atozaye kwa nguvu amekoma; afanyaye ukiwa ametoweka; waliokanyaga watu wametoka katika nchi.
Ezekieli 22 : 12
12 ② Ndani yako wamepokea rushwa ili kumwaga damu; umepokea riba na faida; nawe kwa choyo umepata mapato kwa kuwadhulumu jirani zako, nawe umenisahau mimi, asema Bwana MUNGU.
Mika 3 : 3
3 Naam, mnakula nyama ya watu wangu, na kuwachuna ngozi zao, na kuivunja mifupa yao; naam, kuwakata vipande vipande kama kwa kutiwa chunguni, na kama nyama sufuriani.
Mathayo 23 : 25
25 ⑰ Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi.
Luka 18 : 11
11 ⑭ Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang’anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru.
1 Wakorintho 5 : 11
11 ⑤ Lakini, mambo yalivyo, niliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
Mwanzo 25 : 31
31 Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza.
Mwanzo 47 : 26
26 ⑬ Yusufu akaifanya kuwa sheria ya nchi ya Misri hata leo, ya kwamba sehemu ya tano iwe mali ya Farao. Ila nchi ya makuhani tu haikuwa mali ya Farao.
Leave a Reply