Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ukombozi
Zaburi 34 : 17
17 Walilia, naye BWANA akasikia, Akawaponya kutoka kwa taabu zao zote.
Zaburi 107 : 6
6 ⑧ Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao.
2 Samweli 22 : 2
2 akasema, BWANA ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu,
Zaburi 50 : 15
15 Uniite siku ya mateso; Nitakuokoa, nawe utanitukuza.
Yakobo 5 : 16
16 Basi ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, ili mpate kuponywa. Sala yake mwenye haki ina nguvu nyingi, na hutenda mengi.
Yeremia 1 : 7 – 8
7 Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.
8 Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA.
Warumi 12 : 1 – 2
1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
2 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.
Zaburi 34 : 4
4 ② Nilimtafuta BWANA, naye akanijibu, Akaniokoa kutoka kwa hofu zangu zote.
2 Petro 2 : 9
9 basi, Bwana ajua kuwaokoa watauwa na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu;
1 Wakorintho 6 : 18
18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.
Warumi 6 : 14 – 19
14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.
15 Ni nini basi? Tufanye dhambi kwa sababu hatuwi chini ya sheria bali chini ya neema? La hasha!
16 Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa nafsi zenu kuwa watumwa wake katika kumtii, mmekuwa watumwa wake yule mnayemtii, iwe ni utumishi wa dhambi uletao mauti, au iwe ni utumishi wa utii uletao haki.
17 Lakini Mungu na ashukuriwe, kwa maana mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mliitii kwa mioyo yenu ile namna ya elimu ambayo mliwekwa chini yake;
18 na mlipokwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, mkawa watumwa wa haki.
19 Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa.
Wagalatia 5 : 1
1 Katika uhuru huo Kristo alituweka huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.
Yohana 3 : 16
16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Yohana 8 : 32
32 tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru.
Zaburi 40 : 13
13 Ee BWANA, uwe radhi kuniokoa, Ee BWANA, unisaidie hima.
Yohana 15 : 7
7 Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo nanyi mtatendewa.
1 Wakorintho 6 : 9 – 10
9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
10 ⑪ wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.
Zaburi 40 : 17
17 Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie.
Mathayo 10 : 1
1 Akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kuponya magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
Marko 16 : 17
17 ③ Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
Leave a Reply