Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ukaldayo
Mwanzo 11 : 28
28 Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo.
Mwanzo 11 : 31
31 Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
Mwanzo 15 : 7
7 Kisha akamwambia, Mimi ni BWANA, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili uimiliki.
Isaya 23 : 13
13 Tazama, nchi ya Wakaldayo; watu hao hawako tena; Mwashuri ameiweka tayari kwa hayawani wa jangwani; wamesimamisha ngome zao za vita, wameyaharibu majumba yake ya enzi, akaufanya kuwa uharibifu.
Leave a Reply