Biblia inasema nini kuhusu Uhakikisho – Mistari yote ya Biblia kuhusu Uhakikisho

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uhakikisho

Waefeso 3 : 12
12 Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini.

2 Timotheo 1 : 12
12 Kwa sababu hiyo nimepatikana na mateso haya, lakini sitahayari; kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.

Waraka kwa Waebrania 10 : 22
22 ⑧ na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.

Waraka kwa Waebrania 6 : 11
11 Nasi twataka sana kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho;

Waraka kwa Waebrania 6 : 19
19 tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia,

1 Yohana 3 : 14
14 ⑰ Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana tunawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti.

1 Yohana 3 : 19
19 Katika hili tutafahamu ya kwamba tu wa kweli, nasi tutaituliza mioyo yetu mbele zake,

1 Yohana 4 : 18
18 Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.

Isaya 32 : 17
17 ⑦ Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.

Wakolosai 2 : 2
2 ③ ili wafarijiwe mioyo yao, wakiunganishwa katika upendo, wakapate utajiri wote wa kufahamu kwa hakika, wapate kujua kabisa siri ya Mungu, yaani, Kristo;

1 Wathesalonike 1 : 5
5 ya kwamba Injili yetu haikuwafikia katika maneno tu, bali na katika nguvu, na katika Roho Mtakatifu, na uthibitifu mwingi; kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.

Zaburi 4 : 3
3 Bali jueni ya kuwa BWANA amejiteulia mtauwa; BWANA husikia nimwitapo.

1 Wathesalonike 1 : 4
4 Kwa maana, ndugu mnaopendwa na Mungu, tunajua uteule wenu;

Ayubu 19 : 25
25 Lakini mimi najua ya kuwa Mteteaji wangu yu hai, Na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi.

Warumi 8 : 16
16 Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu;

1 Yohana 3 : 2
2 ⑥ Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini tunajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo.

Isaya 12 : 2
2 Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu.

1 Yohana 5 : 13
13 ⑤ Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *