Biblia inasema nini kuhusu Udadisi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Udadisi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Udadisi

Mithali 27 : 20
20 Kuzimu na Uharibifu havishibi; Wala macho ya wanadamu hayashibi.

Mhubiri 7 : 21
21 Tena, usitie moyoni mwako maneno yote wasemayo watu; usije ukamsikia mtumishi wako mwenyewe akikutukana.

Mwanzo 3 : 6
6 ⑪ Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alichuma matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.

Mwanzo 18 : 32
32 ③ Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.

Kutoka 19 : 21
21 ⑪ Ndipo BWANA akamwambia Musa, Shuka chini, uwaonye watu wasije wakafanya njia kuja kwa BWANA kutazama, kisha wengi miongoni mwao wakaangamia.

Kutoka 19 : 24
24 BWANA akamwambia, Nenda, ushuke wewe; nawe utakwea, wewe, na Haruni pamoja nawe; lakini wale makuhani na watu wasipenye kumkaribia BWANA, asije yeye akawafurikia juu yao.

Hesabu 4 : 20
20 ⑩ lakini wasiingie wao kupaona mahali pale patakatifu, hata kwa dakika moja, ili wasife.

2 Wafalme 20 : 13
13 ⑫ Hezekia akawasikiliza, akawaonesha nyumba yote yenye vitu vyake vya thamani, fedha, na dhahabu, na manukato, na marhamu ya thamani, na nyumba yenye silaha zake, na vitu vyote vilivyoonekana katika hazina zake. Wala hapakuwa na kitu asichowaonesha Hezekia, katika nyumba yake, wala katika ufalme wake wote.

Danieli 12 : 9
9 Akasema, Nenda zako, Danieli; maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa mhuri, hata wakati wa mwisho.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *