Biblia inasema nini kuhusu Uchafu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Uchafu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Uchafu

Mambo ya Walawi 5 : 3
3 au kama akiugusa uchafu wa binadamu, uchafu wowote ambao kwao amepata unajisi, bila kujua, hapo apatapo kulijua, ndipo atakapokuwa na hatia;

Mambo ya Walawi 7 : 21
21 Kisha mtu awaye yote atakapogusa kitu chochote kilicho najisi, uchafu wa binadamu, au mnyama aliye najisi, au machukizo yoyote yaliyo najisi, kisha akala nyama ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo ni za BWANA, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.

Mambo ya Walawi 17 : 15
15 Tena kila mtu atakayekula nyamafu, au nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, awe ni mzalia au mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini naye atakuwa najisi hadi jioni; ndipo atakapokuwa safi.

Mambo ya Walawi 21 : 15
15 Naye asiwatie unajisi wazawa wake katika watu wake; kwa kuwa mimi ndimi BWANA nimtakasaye.

Mambo ya Walawi 22 : 8
8 Nyamafu au mnyama aliyeraruliwa na wanyama asile, asijitie unajisi kwa hiyo nyama; mimi ndimi BWANA.

Hesabu 5 : 3
3 mtawatoa nje wote, wanaume kwa wanawake, mtawaweka nje ya kambi; ili wasizitie unajisi kambi zao, ambazo mimi naketi katikati yazo.

Hesabu 9 : 11
11 mwezi wa pili, siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni,[16] wataishika; watamla pamoja na mikate isiyotiwa chachu na mboga za uchungu;

Hesabu 31 : 19
19 Nanyi fanyeni matuo yenu nje ya kambi muda wa siku saba; mtu yeyote aliyemwua mtu, na yeyote aliyemgusa mtu aliyeuawa, jitakaseni nafsi zenu siku ya tatu, na siku ya saba, ninyi na mateka yenu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *