Biblia inasema nini kuhusu ubora – Mistari yote ya Biblia kuhusu ubora

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ubora

Wafilipi 4 : 8
8 Hatimaye, ndugu zangu, mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, yatafakarini hayo.

Wafilipi 1 : 9 – 10
9 Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote;
10 mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo;

Danieli 6 : 3
3 Basi Danieli huyo alipata sifa kuliko wakubwa na watawala, kwa kuwa roho bora ilikuwa ndani yake; naye mfalme akaazimu kumweka juu ya ufalme wote.

2 Petro 1 : 3 – 4
3 Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.
4 Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa kutoka kwa uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.

Danieli 5 : 12
12 ⑮ kwa kuwa roho njema kupita kiasi, na maarifa, na ufahamu, na uwezo wa kufasiri ndoto, na kufunua maneno ya fumbo, na kufungua mafundo, zilionekana katika Danieli huyo, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Basi na aitwe Danieli, naye ataionesha tafsiri.

2 Wathesalonike 1 : 1 – 12
1 Paulo, Silwano na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba yetu, na Bwana Yesu Kristo.
2 Neema na iwe kwenu na amani zitokazo kwa Mungu Baba, na kwa Bwana Yesu Kristo.
3 Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.
4 Hata na sisi wenyewe tunaona fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu kwa ajili ya subira yenu, na imani mliyo nayo katika adha zenu zote na dhiki mnazostahimili.
5 Ndiyo ishara hasa ya hukumu iliyo haki ya Mungu, ili mhesabiwe kuwa mwastahili kuuingia ufalme wa Mungu, ambao kwa ajili yake mnateswa.
6 Kwa kuwa ni haki mbele za Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi;
7 na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake,
8 katika muali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu;
9 watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;
10 yeye atakapokuja ili kutukuzwa katika watakatifu wake, na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile, (kwa sababu ushuhuda wetu ulisadikiwa kwenu).
11 Kwa hiyo tunawaombea ninyi sikuzote, ili Mungu wetu awahesabu kuwa mmekustahili kuitwa kwenu, akatimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu;
12 jina la Bwana wetu Yesu litukuzwe ndani yenu, nanyi ndani yake, kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.

2 Timotheo 3 : 16
16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

Isaya 12 : 1 – 6
1 Na katika siku hiyo utasema, Ee BWANA, nitakushukuru wewe; Kwa kuwa ijapokuwa ulinikasirikia, Hasira yako imegeukia mbali, Nawe unanifariji moyo.
2 Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu.
3 Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.
4 Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litangazeni jina lake kuwa limetukuka.
5 Mwimbieni BWANA; kwa kuwa ametenda makuu; Na yajulikane haya katika dunia yote.
6 Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *