Biblia inasema nini kuhusu Ubinafsi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Ubinafsi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ubinafsi

Mwanzo 4 : 9
9 BWANA akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, kwani mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?

Hesabu 32 : 6
6 Musa akawaambia wana wa Gadi na wana wa Reubeni, Je! Ndugu zenu waende vitani nanyi mtaketi hapa?

Zaburi 38 : 11
11 ② Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Na jamaa zangu wanasimama mbali.

Mithali 11 : 26
26 Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake.

Mithali 18 : 17
17 Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa ana haki; Lakini jirani yake huja na kumchunguza.

Mithali 24 : 12
12 Ukisema, Sisi hatukujua hayo; Je! Yeye aipimaye mioyo siye afahamuye? Naye ailindaye nafsi yako siye ajuaye? Je! Hatamlipa kila mtu sawasawa na kazi yake?

Mithali 28 : 27
27 Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu; Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.

Ezekieli 34 : 18
18 Je! Mwaona ya kuwa ni neno dogo ninyi kulishwa malisho mema, hata mkawa hamna budi kukanyaga kwa miguu yenu yaliyosalia? Na kuwa mmekunywa maji yaliyo safi, nanyi hamna budi kuyatibua kwa miguu yaliyobaki?

Mika 3 : 11
11 Wakuu wake huhukumu ili wapate rushwa, na makuhani wake hufundisha ili wapate ijara, na manabii wake hubashiri ili wapate fedha; ila hata hivyo watamtegemea BWANA, na kusema, Je! Hayupo BWANA katikati yetu? Hapana neno baya lolote litakalotufikia.

Hagai 1 : 4
4 Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika?

Hagai 1 : 10
10 Basi, kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake.

Zekaria 7 : 6
6 Na wakati mnapokula chakula na kunywa, je, Hamli kwa ajili ya nafsi zenu, na kunywa kwa ajili ya nafsi zenu?

Malaki 1 : 10
10 Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yoyote mikononi mwenu.

Mathayo 19 : 22
22 Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

Luka 6 : 34
34 Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile.

Warumi 14 : 15
15 Na ndugu yako akichukizwa kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.

Warumi 15 : 3
3 Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Matusi yao waliokutusi wewe yalinipata mimi.

1 Wakorintho 10 : 24
24 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake.

2 Wakorintho 5 : 15
15 tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.

Wagalatia 6 : 2
2 Mchukuliane mizigo na hivyo kuitimiza sheria ya Kristo.

Wafilipi 2 : 4
4 Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.

Wafilipi 2 : 21
21 ⑦ Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu.

2 Timotheo 3 : 4
4 ⑪ wasaliti, wakaidi, wenye kujivuna, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu;

Yakobo 2 : 16
16 ② na mmoja wenu akawaambia, Nendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya kimwili, yafaa nini?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *