Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia uanaume
1 Wakorintho 16 : 13
13 ⑩ Kesheni, simameni imara katika imani, iweni na ujasiri, mkawe hodari.
1 Wakorintho 13 : 11
11 Nilipokuwa mtoto mchanga, nilisema kama mtoto mchanga, nilifahamu kama mtoto mchanga, nilifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.
1 Wafalme 2 : 1 – 2
1 ② Basi siku ya kufa kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe, akasema,
2 ③ Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujioneshe kuwa shujaa na hodari;
Ayubu 38 : 3
3 Basi jifunge viuno kama mwanamume, Maana nitakuuliza neno, nawe niambie.
Leave a Reply