Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Tamaa
Hesabu 16 : 13
13 je! Ni jambo dogo, wewe kutuleta kutoka nchi iliyobubujika na maziwa na asali, ili kutuua jangwani, lakini pamoja na haya wajikuza mwenyewe uwe mkuu juu yetu kabisa?
2 Wafalme 14 : 9
9 ⑬ Naye Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, Mbaruti uliokuwako Lebanoni ulituma kwa mwerezi uliokuwako Lebanoni, kusema, Umwoze mwanangu binti yako; kukapita hayawani aliyekuwako Lebanoni, akaukanyaga ule mbaruti.
Ayubu 20 : 7
7 Hata hivyo ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe; Hao waliomwona watasema, Yuko wapi?
Zaburi 49 : 13
13 Hiyo ndiyo njia yao, ujinga wao, Nao walioko baada yao huyaridhia maneno yao.
Isaya 5 : 8
8 ⑮ Ole wao waongezao nyumba baada ya nyumba, na kuweka shamba karibu na shamba, hadi ikawa hapana nafasi tena, nanyi ikawa hamna budi kukaa peke yenu katikati ya nchi!
Habakuki 2 : 6
6 Je! Hawa wote hawatapiga mfano juu yake, na mithali ya kusimanga juu yake, wakisema, Ole wake yeye aongezaye kisicho mali yake! Hata lini? Na ole wake yeye ajitwikaye mzigo wa rehani!
Habakuki 2 : 9
9 Ole wake yeye aipatiaye nyumba yake mapato mabaya, ili apate kukiweka kiota chake juu, apate kujiepusha na mkono wa uovu!
Mathayo 4 : 10
10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.
Luka 4 : 8
8 ⑳ Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.
Mathayo 16 : 26
26 Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kuipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Luka 9 : 25
25 Kwa kuwa inamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akajiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?
Mathayo 23 : 7
7 na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi.
Marko 12 : 39
39 na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele katika karamu;
Luka 11 : 43
43 Ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwapenda kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni.
Mathayo 23 : 12
12 ⑫ Na yeyote atakayejikweza, atadhiliwa; na yeyote atakayejidhili, atakwezwa.
Marko 9 : 37
37 Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.
Luka 22 : 24
24 ⑮ Yakatokea mashindano kati yao, kwamba ni nani anayehesabiwa kuwa mkubwa.
Mathayo 18 : 1
1 Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema,
Luka 9 : 46
46 ⑭ Wakaanza kuhojiana, ni nani atakayekuwa mkubwa miongoni mwao.⑮
Marko 10 : 45
45 Kwa maana Mwana wa Adamu naye hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Mathayo 20 : 20
20 Ndipo mama yao wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akamsujudia, na kumwomba kitu.
Luka 22 : 26
26 ⑰ lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye.
Yohana 5 : 44
44 Mnawezaje kuamini ninyi mnaopokeana utukufu ninyi kwa ninyi, na utukufu ule utokao kwa Mungu aliye wa pekee hamwutafuti?
1 Timotheo 3 : 1
1 ③ Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu,[2] atamani kazi njema.
Leave a Reply