Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia subira
Warumi 12 : 12
12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; mkidumu katika kusali;
Wagalatia 6 : 9
9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho.
Warumi 8 : 25
25 Bali tukikitumainia kitu tusichokiona, twakingojea kwa subira.
Zaburi 37 : 7 – 9
7 Utulie mbele za BWANA, Nawe umngojee kwa subira; Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake, Wala mtu apangaye maovu.
8 Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.
9 Maana watenda mabaya watakatiliwa mbali, Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi.
Yeremia 29 : 11
11 Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.
Wafilipi 4 : 6
6 Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
Mhubiri 7 : 9
9 ② Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
Waefeso 4 : 2
2 kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo;
1 Wakorintho 13 : 4
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
1 Petro 2 : 19 – 23
19 Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo pasipo haki.
20 ⑰ Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.
21 ⑱ Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.
22 ⑲ Yeye hakutenda dhambi, wala udanganyifu haukuwapo kinywani mwake.
23 ⑳ Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.
Warumi 5 : 4
4 na kazi ya subira ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini;
Yakobo 1 : 19
19 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika;
Mithali 15 : 18
18 Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.
Isaya 40 : 31
31 bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
2 Timotheo 2 : 24
24 ⑥ Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu;
Yakobo 5 : 8
8 Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.
Yakobo 1 : 4
4 Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.
Yakobo 1 : 3
3 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.
Mhubiri 7 : 8
8 ① Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi.
Warumi 5 : 3
3 ⑰ Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta subira;
Leave a Reply