Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia sifa
Zaburi 100 : 1 – 5
1 Mshangilieni BWANA, enyi nchi zote;
2 Mtumikieni BWANA kwa furaha; Njoni mbele zake mkiimba;
3 Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake;
5 Maana BWANA ni mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake katika vizazi vyote.
Zaburi 150 : 1 – 6
1 Haleluya. Msifuni Mungu katika patakatifu pake; Msifuni katika anga la uweza wake.
2 Msifuni kwa matendo yake makuu; Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;
4 Msifuni kwa matari na kucheza; Msifuni kwa zeze na filimbi;
5 Msifuni kwa matoazi yaliayo; Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6 ① Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya.
Zaburi 147 : 1 – 20
1 Haleluya. Msifuni Bwana; Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu sifa, Maana ni mwenye fadhili, na anastahili kuimbiwa sifa.
2 ⑳ BWANA ndiye aijengaye Yerusalemu, Huwakusanya waliotawanyika wa Israeli.
3 Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuyaganga majeraha yao.
4 Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina.
5 Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka.
6 BWANA huwategemeza wenye upole, Huwaangusha chini wenye jeuri.
7 Mwimbieni BWANA kwa kushukuru, Mwimbieni Mungu wetu kwa kinubi.
8 Huzifunika mbingu kwa mawingu, Huitengenezea nchi mvua, Na kuichipusha nyasi milimani.
9 Humpa mnyama chakula chake, Wana-kunguru waliao.
10 Hapendezwi na nguvu za farasi, Wala hairidhii miguu ya mkimbiaji.[28]
11 BWANA huwaridhia wao wamchao, Na kuzitarajia fadhili zake.
12 Msifu BWANA, Ee Yerusalemu; Msifu Mungu wako, Ee Sayuni.
13 Maana amevikaza vipingo vya malango yako, Amewabariki wanao ndani yako.
14 Ndiye aletaye amani mipakani mwako, Hukushibisha kwa ngano safi.
15 Huipeleka amri yake juu ya nchi, Neno lake lapiga mbio sana.
16 Ndiye atoaye theluji kama sufu, Huimwaga barafu yake kama majivu,
17 Hutupa mvua ya mawe kama makombo, Mbele ya baridi yake ni nani awezaye kusimama?
18 Hulituma neno lake na kuviyeyusha, Huuvumisha upepo wake, maji yakatiririka.
19 Hulitangaza neno lake kwa Yakobo, Na amri zake na hukumu zake kwa Israeli.
20 Hakulitendea taifa lolote mambo kama hayo, Wala hukumu zake hawakuzijua. Haleluya.
Zaburi 148 : 1 – 14
1 Haleluya. Msifuni BWANA kutoka mbinguni; Msifuni katika mahali palipo juu.
2 Msifuni, enyi malaika wake wote; Msifuni, majeshi yake yote.
3 Msifuni, jua na mwezi; Msifuni, nyota zote zenye mwanga.
4 Msifuni, enyi mbingu za mbingu, Nanyi maji mlioko juu ya mbingu.
5 Na vilisifu jina la BWANA, Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.
6 Amevithibitisha hata milele na milele, Ametoa amri wala haitapita.
7 Msifuni BWANA kutoka nchi, Enyi nyangumi na vilindi vyote.
8 Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke, Upepo wa dhoruba utimizao neno lake.
9 Milima na vilima vyote, Miti yenye matunda na mierezi yote.
10 Hayawani, na wanyama wafugwao, Vitambaavyo, na ndege wenye mbawa.
11 Wafalme wa dunia, na watu wote, Wakuu, na watawala wote wa dunia.
12 Vijana wa kiume, na wanawali, Wazee, na watoto;
13 Na walisifu jina la BWANA, Maana jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.
14 Naye amewainulia watu wake pembe, Sifa za watauwa wake wote; Wana wa Israeli, watu walio karibu naye. Haleluya.
Zaburi 66 : 1 – 20
1 Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote,
2 Imbeni utukufu wa jina lake, Tukuzeni sifa zake.
3 ⑤ Mwambieni Mungu, Matendo yako yatisha kama nini! Kwa ajili ya wingi wa nguvu zako, Adui zako watakuja kunyenyekea mbele zako.
4 ⑥ Nchi yote itakusujudia na kukuimbia, Naam, italiimbia jina lako.
5 ⑦ Njoni myaone matendo ya Mungu; Hutisha kwa mambo awatendayo wanadamu;
6 ⑧ Aligeuza bahari ikawa nchi kavu; Katika mto walivuka kwa miguu; Huko ndiko tulikomfurahia yeye.
7 ⑩ Atawalaye kwa uweza wake milele; Ambaye macho yake yanaangalia mataifa; Hebu wanaoasi wasijitukuze nafsi zao.
8 Enyi mataifa, mtukuzeni Mungu wetu, Itangazeni sauti ya sifa zake;
9 Aliyeiweka nafsi yetu katika uhai, Wala hakuuacha mguu wetu usogezwe.
10 ⑪ Kwa maana umetupima, Ee Mungu, Umetujaribu inavyojaribiwa fedha.
11 Ulituingiza ndani ya wavu, Na kuweka viunoni mwetu mzigo uliotulemea.
12 Uliwapandisha watu Juu ya vichwa vyetu. Tulipitia motoni na majini; Ukatutoa na kutuleta kwenye ufanisi.
13 ⑫ Nitaingia nyumbani mwako na kafara; Nitaondoa kwako nadhiri zangu;
14 Ambazo midomo yangu ilizinena; Kinywa changu kikazisema nilipokuwa taabuni.
15 Kafara za vinono nitakutolea, Pamoja na fukizo la kondoo dume, Nitatoa ng’ombe pamoja na mbuzi.
16 Njoni, sikieni, ninyi nyote mnaomcha Mungu, Nami nitayatangaza aliyonitendea roho yangu.
17 Nilimwita kwa kinywa changu, Na sifa kuu zilikuwa chini ya ulimi wangu.
18 ⑬ Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia.
19 Hakika Mungu amesikia; Ameisikiliza sauti ya maombi yangu.
20 Na ahimidiwe Mungu asiyeyakataa maombi yangu, Wala kuniondolea fadhili zake.
Yakobo 5 : 13
13 Kuna mtu miongoni mwenu anayeteseka? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.
Zaburi 76 : 1 – 12
1 Katika Yuda Mungu amejulikana, Katika Israeli jina lake ni kuu.
2 Kibanda chake pia kiko Salemu, Na maskani yake iko Sayuni.
3 ⑤ Huko ndiko alikoivunja mishale ya uta, Ngao, upanga, na zana za vita.
4 ⑥ Wewe U mwenye fahari na adhama, Toka milima ya mateka.
5 ⑦ Wametekwa wenye moyo thabiti; Wamelala usingizi; Wala hawakuiona mikono yao Watu wote walio hodari.
6 ⑧ Kwa kukemea kwako, Ee Mungu wa Yakobo, Gari na farasi wameshikwa na usingizi mzito.
7 ⑩ Wewe ndiwe utishaye, naam, Wewe; Naye ni nani awezaye kusimama ukasirikapo?
8 Toka mbinguni ulitangaza hukumu; Nchi iliogopa, ikakaa kimya.
9 Mungu aliposimama ili kuhukumu Na kuwaokoa wapole wa dunia wote pia.
10 ⑪ Maana hasira ya binadamu itakusifu, Masalio ya hasira utajifunga kama mshipi.
11 ⑫ Wekeni nadhiri na mziondoe Kwa BWANA, Mungu wenu. Wote wanaomzunguka wamletee hedaya, Yeye astahiliye kuogopwa.
12 ⑬ Yeye huzikata roho za wakuu; Na kuwatisha wafalme wa dunia.
Waraka kwa Waebrania 2 : 12
12 akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa.
Zaburi 118 : 15
15 Sauti ya furaha na wokovu Imo hemani mwao wenye haki; Mkono wa kulia wa BWANA hutenda makuu.
Zaburi 71 : 8
8 Kinywa changu kitajazwa sifa zako, Na heshima yako mchana kutwa.
Zaburi 136 : 1 – 26
1 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
3 Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
4 Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
5 Yeye aliyeumba mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
6 Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
7 Yeye aliyeumba mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
8 Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
9 Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
10 Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wao wa kwanza; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
11 Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
12 Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
13 Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
14 Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
15 Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
16 Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
17 Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
18 Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
19 ① Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
20 ② Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
21 ③ Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
22 Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
23 ④ Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
24 Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
25 ⑤ Yeye akipaye kila kiumbe chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
26 Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Leave a Reply