Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Shobach
2 Samweli 10 : 16
16 Naye Hadadezeri akatuma na kuwaleta Washami waliokuwako ng’ambo ya Mto; nao wakaja Helamu, naye Shobaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri, akawaongoza.
2 Samweli 10 : 18
18 Wakakimbia Washami mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari mia saba, na wapanda farasi elfu arubaini, naye akampiga huyo Shobaki, jemadari wa jeshi lao, hata akafa huko.
1 Mambo ya Nyakati 19 : 16
16 Na Washami walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, wakatuma wajumbe, wakawaleta Washami walioko ng’ambo ya Mto, na Shobaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri, akawaongoza.
1 Mambo ya Nyakati 19 : 18
18 Washami wakakimbia mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami watu wa magari elfu saba, na askari waendao kwa miguu elfu arubaini, akamwua na Shobaki, jemadari wa jeshi.
Leave a Reply