Biblia inasema nini kuhusu sheria – Mistari yote ya Biblia kuhusu sheria

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia sheria

Luka 16 : 17
17 Lakini ni rahisi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati.

Warumi 7 : 12
12 ⑧ Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.

1 Timotheo 1 : 8 – 10
8 Lakini twajua ya kuwa sheria ni njema, kama mtu akiitumia kwa njia iliyo halali;
9 akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu asiye na hatia, bali wavunjao sheria, waasi, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,
10 na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na linginelo lolote lisilopatana na mafundisho ya kweli;

1 Yohana 3 : 4
4 ⑦ Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.

Warumi 7 : 7
7 ④ Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? La hasha! Lakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.

Yakobo 2 : 10
10 Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote.

Zaburi 19 : 7 – 9
7 Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia hekima mtu asiye nayo.
8 Maagizo ya BWANA ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya BWANA ni safi, Huyatia macho nuru.
9 Kicho cha BWANA ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za BWANA ni kweli, Zina haki kabisa.

1 Yohana 5 : 3
3 Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.

Mithali 28 : 4
4 Wao waiachao sheria huwasifu waovu; Bali wao waishikao hushindana nao.

Isaya 33 : 22
22 ⑳ Kwa maana BWANA ndiye mwamuzi wetu; BWANA ndiye mfanya sheria wetu; BWANA ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.

Malaki 4 : 4
4 ⑫ Ikumbukeni Torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.

Warumi 13 : 1
1 Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu.

Mathayo 5 : 17 – 45
17 ⑦ Msidhani ya kuwa nilikuja kuitangua Torati au Manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
18 ⑧ Kwa maana, amin,[1] nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.
19 ⑩ Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
20 Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya Waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
21 ⑪ Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue, na mtu akiua, itampasa hukumu.
22 ⑫ Bali mimi nawaambieni, Kila amkasirikiaye ndugu yake itampasa hukumu; na mtu akimtusi ndugu yake, anastahili kuhukumiwa na baraza; na mtu akimwambia nduguye, Ewe mpumbavu, anastahili kuingia katika moto wa Jehanamu.
23 ⑬ Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako,
24 iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kisha urudi uitoe sadaka yako.
25 ⑭ Patana na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa hakimu, na hakimu akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani.
26 Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hadi utakapolipa senti ya mwisho.
27 ⑮ Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini;
28 ⑯ lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
29 ⑰ Jicho lako la kulia likikukosesha, ling’oe ulitupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee kuliko mwili wako wote utupwe katika Jehanamu.
30 ⑱ Na mkono wako wa kulia ukikukosesha, ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee kuliko mwili wako wote kutupwa katika Jehanamu.
31 ⑲ Imenenwa pia, Mtu akimwacha mkewe, na ampe hati ya talaka;
32 ⑳ lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.
33 Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiape uongo, ila mtimizie Bwana viapo vyako;
34 lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu;
35 wala kwa nchi, kwa maana ndipo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu.
36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
37 Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
38 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili.
40 Na mtu atakaye kukushitaki na kulichukua shati lako, mwachie na koti pia.
41 Mtu yeyote akikulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye maili mbili.
42 Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.
43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

Matendo 7 : 53
53 ninyi mlioipokea torati kwa agizo la malaika msiishike.

Yohana 1 : 17
17 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.

Warumi 13 : 10
10 ⑤ Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *