Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Abibu
Kutoka 12 : 2
2 Mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa mwaka kwenu.
Kutoka 23 : 15
15 Utaiweka sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu; utakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba kama nilivyokuagiza, kwa wakati uliowekwa, mwezi wa Abibu (kwa maana ndio mwezi uliotoka Misri); wala hapana mtu atakayeonekana mbele yangu na mikono mitupu;
Kumbukumbu la Torati 16 : 1
1 ⑰ Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie Pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako.
Kutoka 40 : 2
2 Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza utaisimamisha hiyo maskani ya hema ya kukutania.
Kutoka 40 : 17
17 Hata mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili, siku ya kwanza ya mwezi maskani ile ilisimamishwa.
Hesabu 20 : 1
1 ⑯ Kisha wana wa Israeli, mkutano wote, wakaingia jangwa la Sinai, katika mwezi wa kwanza, watu wakakaa Kadeshi; Miriamu akafa huko, akazikwa huko.
Yoshua 4 : 19
19 Na hao watu wakakwea kutoka Yordani siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, wakapiga kambi Gilgali, katika mpaka wa mashariki wa Yeriko.
1 Mambo ya Nyakati 12 : 15
15 Hao ndio wale waliovuka Yordani katika mwezi wa kwanza, ulipofurika kingo zake zote; nao wakawakimbiza wote wa bondeni kuelekea mashariki na magharibi pia.
Leave a Reply