Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sarah
Mwanzo 11 : 31
31 Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.
Mwanzo 12 : 5
5 Abramu akamchukua Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia na hao watu waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani.
Mwanzo 12 : 20
20 Farao akawaagiza watu kwa ajili yake, wakampeleka njiani, na mkewe, na kila alichokuwa nacho.
Mwanzo 20 : 12
12 Hata hivyo, kwa kweli yeye ni dada yangu, yaani binti wa baba yangu na wala sio binti wa mama yangu; ndipo akawa mke wangu.
Mwanzo 20 : 14
14 Basi Abimeleki akatwaa kondoo, na ng’ombe, na watumwa, na wajakazi, akampa Abrahamu, akamrudishia Sara mkewe.
Mwanzo 16 : 3
3 Kwa hiyo, baada ya Abramu kukaa miaka kumi katika nchi ya Kanaani, Sarai mkewe Abramu alimtwaa Hajiri Mmisri, mjakazi wake, akampa Abramu mumewe, kama mke.
Mwanzo 16 : 6
6 Naye Abramu akamwambia Sarai, Tazama, mjakazi wako yu mikononi mwako, mtendee lililo jema machoni pako. Sarai akamtesa, naye akakimbia kutoka mbele yake.
Mwanzo 21 : 14
14 ⑩ Abrahamu akaamka asubuhi na mapema akatwaa mkate na kiriba cha maji, akampa Hajiri akamtwika begani pake, na kijana, akamruhusu; naye akatoka, akapotea katika jangwa la Beer-sheba.
Mwanzo 17 : 21
21 Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao.
Mwanzo 18 : 15
15 Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo! Umecheka.
Mwanzo 17 : 15
15 Mungu akamwambia Abrahamu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara.
Mwanzo 21 : 3
3 Abrahamu akamwita jina lake Isaka, yule mwana aliyezaliwa, ambaye Sara alimzalia.
Mwanzo 21 : 8
8 Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Abrahamu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.
Leave a Reply