Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Betheli
Yoshua 18 : 13
13 Kisha mpaka ukaendelea kutoka hapo na kufikia mji wa Luzu, ubavuni mwa Luzu (ndio Betheli), kwa upande wa kusini; kisha mpaka ukateremkia Ataroth-adari, karibu na mlima ulio upande wa kusini wa Beth-horoni wa chini.
Waamuzi 1 : 26
26 Huyo mtu akaenda katika nchi ya Wahiti, akajenga mji, akaliita jina la huo mji Luzu; nalo ndilo jina lake hata hivi leo.
Mwanzo 12 : 8
8 Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; Betheli ilikuwa upande wa magharibi, na Ai upande wa mashariki, akamjengea BWANA madhabahu huko, akaliitia jina la BWANA.
Mwanzo 13 : 4
4 ③ napo ndipo palipokuwa na madhabahu aliyofanya hapo kwanza; naye Abramu akaliitia jina la BWANA hapo.
Mwanzo 28 : 22
22 ⑰ Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
Mwanzo 31 : 13
13 Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.
Hosea 12 : 4
4 ⑭ Naam, alishindana na malaika Akashinda; alilia, na kumsihi; Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;
Mwanzo 35 : 15
15 Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.
Mwanzo 35 : 8
8 ⑪ Akafa Debora mlezi wa Rebeka, akazikwa chini ya Betheli, chini ya mwaloni; na jina lake likaitwa Alon-bakuthi.[17]
Yoshua 8 : 17
17 Hakusalia mtu yeyote ndani ya Ai, au katika Betheli, asiyetoka nje kuwafuatia Israeli; wakauacha mji wazi na kuwafuatia Israeli.
Yoshua 12 : 16
16 mfalme wa Makeda, mmoja; na mfalme wa Betheli, mmoja;
Waamuzi 1 : 26
26 Huyo mtu akaenda katika nchi ya Wahiti, akajenga mji, akaliita jina la huo mji Luzu; nalo ndilo jina lake hata hivi leo.
Yoshua 18 : 13
13 Kisha mpaka ukaendelea kutoka hapo na kufikia mji wa Luzu, ubavuni mwa Luzu (ndio Betheli), kwa upande wa kusini; kisha mpaka ukateremkia Ataroth-adari, karibu na mlima ulio upande wa kusini wa Beth-horoni wa chini.
Yoshua 18 : 22
22 na Bethiaraba, na Semaraimu, na Betheli;
Waamuzi 4 : 5
5 Naye alikuwa akikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue.
Leave a Reply