Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Perfume
Mithali 27 : 9
9 Marhamu na manukato huufurahisha moyo; Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake.
Wimbo ulio Bora 3 : 6
6 Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani, Mfano wake ni nguzo za moshi; Afukizwa manemane na ubani, Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?
Isaya 57 : 9
9 Ulimwendea mfalme na mafuta ya marhamu, ukaongeza manukato yako, ukawatuma wajumbe wako waende mbali, ukajidhili sana hadi kuzimu.
Kutoka 30 : 7
7 Na Haruni atafukiza uvumba wa manukato juu yake; kila siku asubuhi atakapozitengeneza zile taa, ataufukiza.
Kutoka 35 : 28
28 ⑤ na viungo vya manukato, na mafuta; kwa hiyo taa, na kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri.
Mithali 7 : 17
17 Nimetia kitanda changu manukato, Manemane na udi na mdalasini.
Isaya 3 : 20
20 na dusumali, na mafurungu, na vitambi, na vibweta vya marashi, na matalasimu;
Leave a Reply