Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia nyumba
Mithali 24 : 3
3 Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika,
Matendo 16 : 31
31 Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.
Waraka kwa Waebrania 3 : 4
4 Maana kila nyumba imetengenezwa na mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu.
Kumbukumbu la Torati 20 : 5
5 Na maofisa na waseme na watu, na kuwaambia, Ni mtu gani aliye hapa aliyejenga nyumba mpya, wala hajaiweka wakfu? Aende akarudi nyumbani kwake, asije akafa mapiganoni, ikawekwa wakfu na mtu mwingine.
Mithali 24 : 4
4 Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza.
Yoshua 24 : 15
15 ⑭ Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA.
Isaya 56 : 7
7 Nitawaleta hao nao hadi katika mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.
Leave a Reply