Biblia inasema nini kuhusu Nyongo – Mistari yote ya Biblia kuhusu Nyongo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Nyongo

Ayubu 16 : 13
13 Wapigaji wake wa mishale hunizingira kotekote, Hunipasua figo zangu, asinihurumie; Nyonga zangu amezimwaga juu ya nchi.

Ayubu 20 : 14
14 ⑫ Hata hivyo chakula chake matumboni mwake kinabadilika, Kimekuwa ni nyongo za majoka ndani yake.

Kumbukumbu la Torati 29 : 18
18 asiwe mtu katikati yenu, mume wala mke, wala jamaa, wala kabila, ageukaye moyo wake leo amwache BWANA, Mungu wetu, kwenda kuitumikia miungu ya mataifa hayo; lisiwe katikati yenu shina lizaalo uchungu na pakanga;

Zaburi 69 : 21
21 Wakanipa uchungu kuwa chakula changu; Na nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki.

Mathayo 27 : 34
34 ④ wakampa kunywa divai iliyochanganyika na nyongo; lakini yeye alipoionja hakutaka kunywa.

Matendo 8 : 23
23 ⑯ Kwa maana nakuona uko katika uchungu kama nyongo, na tena uko katika kifungo cha uovu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *