Biblia inasema nini kuhusu Beer-Sheba – Mistari yote ya Biblia kuhusu Beer-Sheba

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Beer-Sheba

Waamuzi 20 : 1
1 ⑳ Ndipo wana wa Israeli walipotoka; na mkutano ukakutanika kama mtu mmoja, kutoka Dani hadi Beer-sheba, pamoja na nchi ya Gileadi wakamkutanikia BWANA huko Mispa.

Mwanzo 21 : 33
33 Abrahamu akapanda mkwaju huko Beer-sheba, akaliitia huko jina la BWANA Mungu wa milele.

Mwanzo 22 : 19
19 Basi Abrahamu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Abrahamu akakaa huko Beer-sheba.

Mwanzo 26 : 23
23 Akapanda kutoka hapo mpaka Beer-sheba.

Mwanzo 28 : 10
10 ⑦ Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani.

Mwanzo 46 : 1
1 Israeli Akasafiri, pamoja na yote aliyokuwa nayo, akaja Beer-sheba, akamchinjia sadaka Mungu wa Isaka babaye.

Yoshua 15 : 20
20 Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Yuda sawasawa na jamaa zao.

Yoshua 15 : 28
28 Hasar-shuali, Beer-sheba, Biziothia;

2 Samweli 24 : 7
7 wakaja ngomeni kwa Tiro, na kwa miji yote ya Wahivi, na ya Wakanaani; tena wakaenda katika Negebu ya Yuda huko Beer-sheba.

Yoshua 19 : 2
2 ③ Miji waliyokuwa nayo katika urithi wao ni Beer-sheba, Sheba, Molada;

Yoshua 19 : 9
9 Huo urithi wa hao wana wa Simeoni ulitoka katika fungu la wana wa Yuda; kwa maana hilo fungu la wana wa Yuda lilikuwa ni kubwa mno kwao; kwa hiyo wana wa Simeoni walikuwa na urithi katikati ya urithi wao.

1 Mambo ya Nyakati 4 : 28
28 Nao wakakaa huko Beer-sheba, na Molada, na Hasar-shuali;

1 Samweli 8 : 2
2 Na jina la mwanawe mzaliwa wa kwanza lilikuwa Yoeli; na jina la wa pili Abiya; walikuwa waamuzi katika Beer-sheba.

Amosi 5 : 5
5 ⑬ bali msitafute Betheli, wala msiingie Gilgali, wala msipite kwenda Beer-sheba; kwani Gilgali hakika yake itakwenda utumwani, na Betheli itakuwa ubatili.

Amosi 8 : 14
14 Na hao waapao kwa dhambi ya Samaria, na kusema, Kama aishivyo Mungu wako, Ee Dani, na, Kama iishivyo njia ya Beer-sheba, hao nao wataanguka, wasiinuke tena.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *