Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ngao
Zaburi 35 : 2
2 Uishike ngao na kikingio, Uinuke unisaidie.
Ezekieli 38 : 4
4 nami nitakugeuza na kutia kulabu katika mataya yako, nami nitakutoa, pamoja na jeshi lako lote, farasi na hao wapandao farasi, wote wamevaa silaha za namna zote, jeshi kubwa sana, wenye ngao na kigao, wote wakishika upanga;
2 Samweli 1 : 21
21 Enyi milima ya Gilboa, visiwepo juu yenu Umande wala mvua, wala mashamba ya matoleo; Maana ndipo ilipotupwa kwa aibu ngao ya shujaa, Ngao yake Sauli, pasipo kutiwa mafuta.
2 Mambo ya Nyakati 14 : 8
8 Naye Asa alikuwa na jeshi waliochukua ngao na mikuki, katika Yuda elfu mia tatu; na katika Benyamini wenye kuchukua vigao na kupinda upinde, elfu mia mbili na themanini; hao wote walikuwa mashujaa.
2 Mambo ya Nyakati 17 : 17
17 na wa Benyamini; Eliada mtu shujaa, na pamoja naye elfu mia mbili wenye nyuta na ngao;
2 Mambo ya Nyakati 26 : 14
14 Uzia akawapatia jeshi lote ngao na mikuki, na chapeo, na deraya za madini, na nyuta, na mawe ya kupiga kwa teo.
1 Wafalme 14 : 27
27 Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba mahali pake, akawakabidhi wakuu wa walinzi, waliongoja mlangoni pa nyumba ya mfalme.
2 Samweli 8 : 7
7 Tena Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizovaliwa na watumishi wa Hadadezeri, akazileta Yerusalemu.
1 Wafalme 10 : 17
17 Na vigao mia tatu vya dhahabu iliyofuliwa; kila kigao kimoja kilipata mane tatu za dhahabu. Mfalme akaviweka katika nyumba ya msitu wa Lebanoni.
2 Mambo ya Nyakati 9 : 16
16 Na vigao mia tatu vya dhahabu iliyofuliwa; kigao kimoja hupata shekeli mia tatu za dhahabu; mfalme akaviweka katika nyumba ya msitu wa Lebanoni.
Ezekieli 39 : 10
10 hata hawataokota kuni mashambani, wala hawatakata kuni msituni; maana watafanya mioto kwa silaha zile; nao watawateka nyara watu waliowateka wao, na kuwapora watu waliowapora wao, asema Bwana MUNGU.
Ayubu 15 : 26
26 Humshambulia na shingo ngumu, Kwa mafundo makubwa ya ngao zake;
2 Wafalme 10 : 17
17 ② Naye alipofika Samaria, aliwaua wote wa Ahabu waliokuwa wamebakia katika Samaria, hata akamwangamiza, sawasawa na neno la BWANA alilomwambia Eliya.
2 Mambo ya Nyakati 11 : 12
12 Na ndani ya miji yote mmoja mmoja aliweka ngao na mikuki, akaifanya kuwa na nguvu nyingi mno. Yuda na Benyamini ikawa milki yake.
2 Mambo ya Nyakati 32 : 5
5 ⑪ Hezekia akapiga moyo konde, akaujenga ukuta wote uliobomoka, akauinua sawa na minara, na ukuta wa pili nje, akaongeza nguvu ya Milo, katika mji wa Daudi, akafanya silaha na ngao tele.
2 Mambo ya Nyakati 32 : 27
27 Naye Hezekia akawa na mali nyingi mno na heshima; akajitengenezea hazina za fedha, za dhahabu, za vito, za manukato, za ngao, na za namna zote za vyombo vya thamani;
2 Wafalme 11 : 10
10 ⑳ Naye yule kuhani akawapa wakuu wa mamia mikuki na ngao zilizokuwa za mfalme Daudi, zilizokuwamo nyumbani mwa BWANA.
2 Mambo ya Nyakati 23 : 9
9 Naye Yehoyada kuhani akawapa makamanda wa mamia mikuki, na ngao, na vigao, vilivyokuwa vya mfalme Daudi, vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu.
Leave a Reply