Biblia inasema nini kuhusu Necromancy – Mistari yote ya Biblia kuhusu Necromancy

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Necromancy

Kumbukumbu la Torati 18 : 11
11 ⑬ wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu.

Kumbukumbu la Torati 26 : 14
14 katika vitu hivyo sikula wakati wa kukaa matanga mimi, wala sikuviondoa nikiwa na unajisi, wala sikutoa kwa ajili ya wafu katika vitu hivyo; sauti ya BWANA, Mungu wangu, nimeisikiza, nimefanya yote, kama ulivyoniamuru.

Isaya 8 : 19
19 ③ Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?

Isaya 29 : 4
4 ⑦ Nawe utashushwa, nawe utanena toka chini ya nchi, na maneno yako yatakuwa chini toka mavumbini; na sauti yako itakuwa kama sauti ya mtu mwenye pepo, ikitoka katika nchi, na matamko yako yatanong’ona toka mavumbini.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *