Biblia inasema nini kuhusu Nathan – Mistari yote ya Biblia kuhusu Nathan

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Nathan

2 Samweli 5 : 14
14 Na haya ndiyo majina ya hao waliozaliwa kwake huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani,

1 Mambo ya Nyakati 3 : 5
5 Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu;

1 Mambo ya Nyakati 14 : 4
4 Na haya ndiyo majina ya watoto aliozaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani;

2 Samweli 7 : 17
17 Kwa maneno hayo yote, na kwa maono hayo yote, ndivyo Nathani alivyonena na Daudi.

1 Mambo ya Nyakati 17 : 15
15 Kwa maneno hayo yote, na kwa maono hayo yote, ndivyo Nathani alivyonena na Daudi.

2 Samweli 12 : 15
15 ③ Naye Nathani akaondoka kwenda nyumbani kwake. Basi BWANA akampiga yule mtoto ambaye mkewe Uria alimzalia Daudi naye akawa mgonjwa sana.

2 Samweli 12 : 25
25 akapeleka kwa mkono wa Nathani, nabii, naye akamwita jina lake Yedidia,[9] kwa ajili ya BWANA.

1 Wafalme 1 : 14
14 Tazama, wakati ule utakapokuwa katika kusema na mfalme, mimi nami nitaingia nyuma yako, na kuyahakikisha maneno yako.

1 Wafalme 1 : 27
27 Je! Bwana wangu mfalme ndiye aliyelitenda jambo hili, bila kutujulisha sisi watumishi wako ni nani atakayeketi katika kiti cha enzi cha bwana wangu mfalme baada yake?

1 Wafalme 1 : 45
45 Kisha Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, wakamtia mafuta huko Gihoni, ili awe mfalme. Nao wamepanda juu kutoka huko wakifurahi, hata mji ukavuma. Ndizo kelele zile mlizozisikia.

1 Mambo ya Nyakati 29 : 29
29 Basi habari za mfalme Daudi, mwanzo hadi mwisho, angalia, zimeandikwa katika kumbukumbu za Samweli, mwonaji, na katika kumbukumbu za Nathani, nabii, na katika kumbukumbu za Gadi, mwonaji;

2 Mambo ya Nyakati 9 : 29
29 ⑰ Basi mambo yake Sulemani yaliyosalia, tangu mwanzo hadi mwisho je! Hayakuandikwa katika kitabu cha kumbukumbu la Nathani nabii, katika unabii wa Ahiya, Mshiloni, na katika maono ya Ido mwonaji ambayo yahusu Yeroboamu mwana wa Nebati?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *