Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia nabii mke
Kutoka 15 : 20
20 Na Miriamu, nabii mwanamke, dada yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.
Luka 2 : 36 – 38
36 Palikuwa na nabii mwanamke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.
37 Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.
38 Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.
Luka 2 : 36
36 Palikuwa na nabii mwanamke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake.
Wagalatia 3 : 28
28 Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.
2 Wafalme 22 : 14
14 Basi Hilkia kuhani, na Ahikamu, na Akbori, na Shafani, na Asaya, wakamwendea Hulda, nabii wa kike, mkewe Shalumu, mwana wa Tikva, mwana wa Harhasi, mtunza mavazi ya mfalme; (naye alikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili;) wakasema naye.
Matendo 2 : 17 – 18
17 ① Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.
18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri.
Waamuzi 4 : 4
4 Basi Debora, nabii mwanamke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule.
Matendo 21 : 9
9 Mtu huyu alikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiri.
Kutoka 15 : 20 – 21
20 Na Miriamu, nabii mwanamke, dada yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.
21 Miriamu akawaitikia, Mwimbieni BWANA kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.
1 Wakorintho 14 : 3
3 Bali yeye ahutubuye, asema na watu maneno ya kuwajenga, na kuwafariji, na kuwatia moyo.
Isaya 8 : 3
3 Nami nikalala na nabii mwanamke, naye akapata mimba, akazaa mtoto wa kiume. Kisha BWANA akaniambia, Mwite jina lake Maher-shalal-hash-bazi.
Waamuzi 4 : 9
9 Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana BWANA atamwuza Sisera katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi.
Waamuzi 4 : 1 – 24
1 Hata alipokufa Ehudi, wana wa Israeli wakafanya yaliyo maovu tena mbele za macho ya BWANA.
2 BWANA akawauza na kuwatia katika mkono wa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori; na Sisera, aliyekaa katika Haroshethi wa Mataifa, alikuwa kamanda wa jeshi lake.
3 Wana wa Israeli wakamlilia BWANA; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia tisa ya vita;[6] naye akawakandamiza sana wana wa Israeli muda wa miaka ishirini.
4 Basi Debora, nabii mwanamke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule.
5 Naye alikuwa akikaa chini ya mtende wa Debora, kati ya Rama na Betheli, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu; wana wa Israeli wakakwea kwake, awaamue.
6 Siku moja Debora akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu kutoka Kedesh-Naftali, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli anakuamuru hivi: “Nenda, ukawaogoze watu elfu kumi na wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni, ili washike doria katika mlima Tabori”.
7 Nami nitakuvutia Sisera, kamanda wa jeshi la Yabini, hadi mto wa Kishoni, pamoja na magari yake, na wingi wa watu wake; nami nitamtia mkononi mwako.
8 Baraka akamwambia, Kama utakwenda pamoja nami ndipo nitakwenda; bali kama huendi pamoja nami, mimi siendi.
9 Basi akasema, Hakika nitakwenda pamoja nawe, lakini safari utakayoiendea haitakupatia heshima wewe; maana BWANA atamwuza Sisera katika mkono wa mwanamke. Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka mpaka Kedeshi.
10 Baraka akawakutanisha Naftali na Zabuloni waende Kedeshi wakakwea watu elfu kumi wakimfuata; Debora naye akaenda pamoja naye.
11 Basi Heberi, Mkeni,[7] alikuwa amejitenga na Wakeni, yaani na wana wa Hobabu, shemeji yake Musa, akaipiga hema yake mbali penye mwaloni ulioko Saananimu, karibu na Kedeshi.
12 Watu wakamwambia Sisera ya kwamba Baraka, mwana wa Abinoamu amekwea kwenda mlima wa Tabori.
13 Sisera akayakusanya magari yake yote, naam, magari ya chuma mia tisa, na watu wote waliokuwa pamoja naye, toka Haroshethi wa Mataifa mpaka mto wa Kishoni.
14 Debora akamwambia Baraka, Haya! Inuka; maana siku hii ndiyo siku ambayo BWANA amemtia Sisera katika mkono wako. Je! BWANA hakutoka atangulie mbele yako? Basi Baraka akashuka katika mlima wa Tabori, na watu elfu kumi wakamfuata.
15 BWANA akamfadhaisha Sisera na magari yake yote, na jeshi lake lote, kwa makali ya upanga, mbele ya Baraka; basi Sisera akashuka katika gari lake, akakimbia kwa miguu.
16 Lakini Baraka akayafuatia magari, na jeshi, hadi Haroshethi wa Mataifa; na hilo jeshi lote la Sisera likaanguka kwa makali ya upanga; hakusalia hata mtu mmoja.
17 Lakini Sisera akakimbia kwa miguu, akaifikia hema ya Yaeli mkewe Heberi, Mkeni; kwa maana palikuwa na amani kati ya Yabini, mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi, Mkeni.
18 Yaeli akatoka kwenda kumlaki Sisera, akamwambia, Karibu Bwana wangu, karibu kwangu; usiogope. Akakaribia kwake hemani, naye akamfunika kwa bushuti.
19 Akamwambia, Tafadhali nipe maji kidogo ninywe; maana nina kiu. Akafungua chupa ya maziwa, akampa kunywa, akamfunika.
20 Naye akamwambia, Simama mlangoni pa hema; kisha itakuwa mtu yeyote akija na kukuuliza, akisema, Je! Yupo mtu hapa, basi, mjibu, La, hapana.
21 ① Ndipo Yaeli, mkewe Heberi, akatwaa kigingi cha hema, akashika nyundo mkononi mwake, akamwendea polepole, akamtia kile kigingi katika kipaji chake, nacho kikapenya, hata kuingia mchangani; kwa maana usingizi mzito ulikuwa umemshika; basi akazimia, akafa.
22 Na tazama, Baraka alipokuwa akimfuatia Sisera; Yaeli akatoka ili kumlaki, akamwambia, Njoo, nami nitakuonesha yule mtu unayemtafuta. Basi akamwendea, na tazama, Sisera amelala humo, amekufa, na hicho kigingi kilikuwa kipajini mwake.
23 ② Basi hivyo Mungu akamshinda Yabini, mfalme wa Kanaani mbele ya wana wa Israeli siku hiyo.
24 Mkono wa wana wa Israeli ukazidi kupata nguvu juu ya Yabini, mfalme wa Kanaani, hata walipokuwa wamemwangamiza Yabini, mfalme wa Kanaani.
Warumi 16 : 1
1 Namkabidhi kwenu Fibi, dada yetu, aliye mhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea;
Leave a Reply