Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mtu anayemwamini
Zaburi 118 : 8
8 ⑧ Ni heri kumkimbilia BWANA Kuliko kuwatumainia wanadamu.
Mika 7 : 5 – 8
5 Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari.
6 Kwa maana mwana humwaibisha babaye, na binti huondoka ashindane na mamaye; na mwanamke aliyeolewa hushindana na mavyaaye; adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake mwenyewe.
7 Lakini mimi, nitamtazamia BWANA; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia.
8 Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo, nitasimama tena; nikaapo gizani, BWANA atakuwa nuru kwangu.
Yeremia 9 : 4
4 ⑤ Jihadharini, kila mtu na jirani yake, wala msimtumaini ndugu awaye yote; maana kila ndugu atachongea, na kila jirani atakwenda huku na huko na kusingizia.
Isaya 2 : 22
22 ② Mwacheni mwanadamu ambaye pumzi yake iko katika mianzi ya pua yake; kwa maana wanafaa kitu gani?
Yeremia 17 : 5 – 6
5 BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.
6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
Mika 7 : 5 – 6
5 Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari.
6 Kwa maana mwana humwaibisha babaye, na binti huondoka ashindane na mamaye; na mwanamke aliyeolewa hushindana na mavyaaye; adui za mtu ni watu wa nyumbani mwake mwenyewe.
Mithali 28 : 26
26 Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga; Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa.
Zaburi 146 : 3
3 ⑯ Msiwatumainie wakuu, Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.
Zaburi 118 : 9 – 13
9 ⑩ Ni heri kumkimbilia BWANA. Kuliko kuwatumainia wakuu.
10 Mataifa yote walinizunguka; Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali.
11 ⑪ Walinizunguka, naam, walinizunguka; Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali.
12 ⑫ Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali.
13 Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini BWANA akanisaidia.
Zaburi 40 : 3 – 4
3 Akatia wimbo mpya kinywani mwangu, Ndio sifa zake Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, Nao watamtumainia BWANA.
4 ⑭ Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo.
Mithali 25 : 26
26 Mwenye haki amwangukiapo mtu mbaya Ni kama chemchemi iliyochafuka, Na kisima kilichokanyagwa.
Yohana 14 : 15
15 ⑬ Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
Yohana 2 : 24 – 25
24 Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote;
25 na kwa sababu hakuwa na haja ya mtu kushuhudia habari za mwanadamu; kwa maana yeye mwenyewe alijua yaliyomo ndani ya mwanadamu.
Leave a Reply