Biblia inasema nini kuhusu Balaki – Mistari yote ya Biblia kuhusu Balaki

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Balaki

Hesabu 22 : 4
4 ⑲ Moabu akawaambia wazee wa Midiani, Sasa jeshi hili la watu litaramba vitu vyote vinavyotuzunguka, kama vile ng’ombe arambavyo majani ya mashamba. Na Balaki, mwana wa Sipori, alikuwa mfalme wa Moabu zamani zile.

Yoshua 24 : 9
9 ⑦ Ndipo Balaki, mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu, akainuka, akapigana na Israeli; tena akatuma watu kumwita Balaamu, mwana wa Beori, aje awalaani;

Waamuzi 11 : 25
25 Na wewe sasa, je! U mwema kuliko Balaki mwana wa Sipori, huyo mfalme wa Moabu, kwa lolote? Je! Yeye alishindana na Israeli, au kupigana nao?

Mika 6 : 5
5 ⑮ Enyi watu wangu, kumbukeni sasa alivyouliza Balaki, mfalme wa Moabu, na alivyojibu Balaamu, mwana wa Beori; kumbukeni yaliyotukia toka Shitimu hadi Gilgali, mpate kuyajua matendo ya haki ya BWANA.

Hesabu 22 : 7
7 Wazee wa Moabu, na wazee wa Midiani, wakaenda, wakichukua ujira wa uganga mikononi mwao; wakamfikia Balaamu, wakamwambia maneno ya Balaki.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *