Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia mitala
Kumbukumbu la Torati 17 : 17
17 Wala asijizidishie wake, ili moyo wake usikengeuke; wala asifanye fedha zake na dhahabu kuwa nyingi mno.
1 Wakorintho 7 : 2
2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe.
1 Timotheo 3 : 12
12 Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao.
Kutoka 21 : 10
10 Akijitwalia mke mwingine, chakula chake huyo, na nguo zake, na ngono yake, hatampunguzia.
2 Mambo ya Nyakati 24 : 1 – 3
1 ⑤ Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala; akatawala miaka arubaini huko Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Sibia wa Beer-sheba.
2 ⑥ Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA siku zote za Yehoyada kuhani.
3 Yehoyada akamwoza wake wawili, naye akazaa watoto wa kiume na wa kike.
1 Timotheo 3 : 2
2 ④ Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkarimu, ajuaye kufundisha;
1 Wafalme 11 : 3
3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wake zake wakamgeuza moyo.
Kumbukumbu la Torati 21 : 15
15 ⑧ Ikiwa mtu ana wake wawili, mmoja ampenda, mmoja hampendi, nao wamemzalia watoto, ampendaye na asiyempenda wote wawili; na yule mzaliwa wa kwanza akiwa ni wa mke asiyependwa;
Mathayo 19 : 4 – 6
4 ⑰ Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mwanamume na mwanamke,
5 ⑱ akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6 ⑲ Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
2 Mambo ya Nyakati 11 : 21
21 Rehoboamu akampenda Maaka binti Absalomu kuliko wakeze wote na masuria yake; (maana alioa wake kumi na wanane, na masuria sitini, akazaa watoto wa kiume ishirini na wanane na mabinti sitini).
1 Wafalme 11 : 4
4 ③ Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.
Waamuzi 8 : 30
30 Gideoni alikuwa na wana sabini waliozawa na mwili wake; kwa maana alikuwa na wake wengi.
2 Mambo ya Nyakati 24 : 3
3 Yehoyada akamwoza wake wawili, naye akazaa watoto wa kiume na wa kike.
2 Samweli 12 : 8
8 nami nikakupa nyumba ya bwana wako, na wake za bwana wako kifuani mwako; nikakupa nyumba ya Israeli na ya Yuda; na kama hayo yangalikuwa machache, ningalikuongezea mambo mengine mengi.
Tito 1 : 6
6 ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii.
2 Mambo ya Nyakati 13 : 21
21 Ila Abiya akapata nguvu, akaoa wake kumi na wanne, akazaa watoto wa kiume ishirini na wawili, na mabinti kumi na sita.
1 Mambo ya Nyakati 3 : 1 – 9
1 Basi hawa ndio wana wa Daudi, aliozaliwa huko Hebroni; Amnoni, mzaliwa wa kwanza, mwana wa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili, Danieli, wa Abigaili, Mkarmeli;
2 wa tatu, Absalomu, mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri; wa nne, Adoniya, mwana wa Hagithi;
3 wa tano, Shefatia, wa Abitali; wa sita, Ithreamu, kwa Egla, mkewe.
4 Sita alizaliwa huko Hebroni; na huko akatawala miaka saba na miezi sita; na huko Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu.
5 Na hawa alizaliwa huko Yerusalemu; Shamua, na Shobabu, na Nathani, na Sulemani, wanne, wana wa Bathsheba, binti Eliamu;
6 na Ibhari, na Elishua, na Elipeleti;
7 na Noga, na Nefegi, na Yafia;
8 na Elishama, na Eliada, na Elifeleti, watu tisa.
9 Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wana wa masuria; na Tamari alikuwa dada yao.
Isaya 4 : 1
1 ⑧ Na siku hiyo wanawake saba watamshika mwanaume mmoja wakisema, Tutakula chakula chetu, na kuvaa nguo zetu wenyewe, lakini tuitwe tu kwa jina lako; utuondolee aibu yetu.
Kumbukumbu la Torati 21 : 15 – 17
15 ⑧ Ikiwa mtu ana wake wawili, mmoja ampenda, mmoja hampendi, nao wamemzalia watoto, ampendaye na asiyempenda wote wawili; na yule mzaliwa wa kwanza akiwa ni wa mke asiyependwa;
16 ⑩ ndipo itakapokuwa ya kwamba siku atakayowarithisha wanawe alivyo navyo, asimweke mwana wa ampendaye kuwa mzaliwa wa kwanza mbele ya mwana wa asiyempenda, naye ndiye mzaliwa wa kwanza huyu;
17 ⑪ lakini amkubali mzaliwa wa kwanza mwana wa yule asiyempenda, kwa kumpa mafungu mawili katika vyote alivyo navyo; kwa maana ndiye mwanzo wa nguvu zake; haki ya mzaliwa wa kwanza ni yake yeye.
Kumbukumbu la Torati 25 : 5 – 10
5 ⑳ Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe.
6 Na iwe, yule mzaliwa wa kwanza atakayemzaa, amfuate nduguye aliyekufa kwa jina lake, lisije likafutwa jina lake katika Israeli.
7 Na yule mtu kwamba hapendi kumtwaa mke wa nduguye, aende huyo mke wa nduguye langoni kwa wazee, akawaambie, Nduguye mume wangu yuakataa kumsimamishia nduguye jina katika Israeli, hataki kunitimizia yampasayo nduguye mume wangu.
8 Ndipo wamwite wazee wa mji wake waseme naye; naye akisimama na kusema, Sitaki mimi kumtwaa mwanamke huyu,
9 ndipo mke wa nduguye amkaribie mbele ya hao wazee, amvue kiatu chake mguuni mwake, na kumtemea mate ya uso; kisha atajibu yule mwanamke, aseme, Mume akataaye kumjengea nduguye nyumba yake na afanywe hivi.
10 Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu.
Leave a Reply